Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mheshimiwa Selemani Jafo, akihutubia
katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wenyeviti wa Walimu Wakuu wa Shule za
Msingi Tanzania Bara kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma
Septemba 30, 2019. "Ameihamasisha benki ya Mwalimu kuytumia fursa ya
mkutano huo kuwashawishi walimu kutumia huduma za benki hiyo."
Baadhi
ya Wenyeviti wa Walimu Wakuu w aShule za Msingi Tanzania Bara
wakisikilkiza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano
huo.
Baadhi
ya Wenyeviti wa Walimu Wakuu w aShule za Msingi Tanzania Bara
wakisikilkiza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano
huo.
Afisa Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa, akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo, akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa baada ya kuhutubia mkutano huo. |
Afisa
Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa
(katikati), akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Wakuu wa
Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA), Bi. Rehema Remole (kushoto) huku
Katibu Mkuu wa TAPSHA, Bi.Fatuma Kalembo akishuhudia wakati wa mkutano
mkuu wa kwanza wa TAPSHA jijini Dodoma Septemba 30, 2019. Mwalimu
Commercial Bank ilitumia fursa hiyo kutoa elimu ya fedha na
kuwafahamisha walimu umuhimu w akutumia huduma za benki hiyo ambayo
zaidi ya asilimia 50 ya umiliki wa benki hiyo uko chini ya walimu na
chama cha walimu Tanzania (CWT)
Bw. Makungwa akizunhuzma jambo na
Mwalimu Mselemu kutoka Mkoani Singida. Katikati ni Kaimu Mkuu wa
Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank, Bi. Leticia Ndongole.
Afisa
Mtendaji Mkuu, Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa
(katikati), akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Wakuu wa
Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA), Bi. Rehema Ramole (kushoto) huku
Katibu Mkuu wa TAPSHA, Bi.Fatuma Kalembo akishuhudia wakati wa mkutano
mkuu wa kwanza wa TAPSHA jijini Dodoma Septemba 30, 2019. Mwalimu
Commercial Bank ilitumia fursa hiyo kutoa elimu ya fedha na
kuwafahamisha walimu umuhimu w akutumia huduma za benki hiyo ambayo
zaidi ya asilimia 50 ya umiliki wa benki hiyo uko chini ya walimu na
chama cha walimu Tanzania (CWT)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Jafo, amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kote nchini, kutumia posho maalum ya madaraka ya... Mwalimu Mkuu (Responsibility Allowance) kuziwekeza benki ili hatimaye wajiinue kiuchumi kabla ya kustaafu.
Mheshimiwa Jafo ameyasema hayo
jijini Dodoma Jumatatu Septemba 30, 2019 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA) ambapo
Wenyeviti wa Walimu Wakuu kutoka mikoa na wilaya waliwawakilisha wenzao.
“Leo hii kwa mara ya kwanza
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi mnapata posho maalum ya madaraka ya Mwalimu
Mkuu (Responsibility allowance), shilingi 200,000/= kila mwezi, unaweza kuamua
posho yako usiiguse na ukaenda Mwalimu Commercial Bank ukawaambia jamani
niwekeeni posho yangu hii nataka baadaye nijenge nyumba.” Aliwaasa walimu……na
kuongeza... “Nyie watu wa benki watafuteni walimu hawa muelewane nao, hatutaki
mwalimu ajenge nyumba mpaka anapostaafu, sasa muwawezeshe walimu wetu wajenge
nyumba,hata kabla ya mambo mengine na nyie watu wa benki mna fursa hiyo na leo
mpo na wenyeviti wa wakuu wa shule wapo, hapa kipa katoka goli liko
wazi…elewaneni nao leo hapa hapa tunataka hawa walimu kutokana na responsibility
allowance mwalimu apate kajumba kake na inawezekana” Alisema Mhe. Jafo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa aliwahakikishia
walimu kuwa benki hiyo ambayo ilianzishwa na walimu miaka mitatu iliyopita
imekuwa ikiimarika siku hadi siku ambapo miundombinu ya benki imekuwa imara
kuna huduma mbalimbali kama vile Mobile banking (kuweka fedha kwenye
akaunti kupitia mtandao wa simu), lakini pia kuweka mawakala kwenye maeneo
mbalimbali ili kuwafikishia huduma kwa urahisi.
“Ninyi wenyewe kama wadau wakwanza wakubwa mishahara yenu ipitishieni kwenye benki yenu, msiwe kama mtu mmoja aliyekuwa na hamu ya kuanzisha mgawaha, baada ya kuanzisha mgahawa badala ya kula kwenye mgahawa wake akawa anakula kwenye mgahawa wa jirani, chombo chenu mnatakiwa kukitunza kama vile mnavyoitunza taaluma yenu ili baadaye kiwe na manufaa.” Alisema Bw. Makungwa |
No comments:
Post a Comment