Pages

Monday, September 30, 2019

MAHITAJI YA CHAKULA KUONGEZEKA KWA ASILIMIA 60 IFIKAPO MWAKA 2050


Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba akizungumza na waandishi wa habari kwenye ufunguzi wa mkutano wa kuwasilisha kwa Wabia wa Maendeleo mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kupunguza Upotevu wa Mazao kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Kizenga Makumbusho jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba akiungua mkutano wa kuwasilisha kwa Wabia wa Maendeleo mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kupunguza Upotevu wa Mazao kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Kizenga Makumbusho jijini Dar es salaam.
Bw. Clespin Josephat Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC) akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kizenga Makubusho jijini Dar es salaam.
Felix Bachmann Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la HELVETAS akiwasilisha mada katiia mkutano huo.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba akwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo  uliofanyika ukumbi wa Kizenga Makumbusho jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba akwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo  uliofanyika ukumbi wa Kizenga Makumbusho jijini Dar es salaam.
………………………………………………
Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na watu bilioni tisa (9) hivyo mahitaji ya
chakula yanakadiriwa kuwa asilimia 60 zaidi ya ilivyo sasa.
Ameyasema hayo leo Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Omary Mgumba kwenye ufunguzi wa mkutano wa kuwasilisha kwa Wabia wa Maendeleo mpango kazi wa utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kupunguza Upotevu wa Mazao.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Mh.Mgumba amesema Mahitaji ya chakula yanakadiriwa kuwa asilimia 60 zaidi ya ilivyo sasa.
“Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Umoja wa mataifa umedhamiria kutokomeza baa la njaa kwa kuhakikisha kuna usalama wa chakula na lishe, kupunguza upotevu wa mazao na kukuza kilimo endelevu ifikapo mwaka 2030”. Amesema Mh.Mgumba.
Aidha, Mh.Mgumba amesema kuwa mkazo umewekwa katika kuongeza uzalishaji wenye tija wa mazao ya chakula ili kufikia malengobendelevu ya maendeleo.
” Udhibiti wa upotevu wa mazao ya chakula ni suala muhimu na la kipekee ambapo linapaswa kupewa kipaumbele ili kufikia malengo hayo”. Ameeleza Mh.Mgumba.
Pamoja na hayo, Mh.Mgumba amesema kuwa Usalama wa chakula ni moja ya lengo kuu la Wizara ya Kilimo katika kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Viwanda ili kutekeleza agenda kuu ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mh.Dkt.John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment