Pages

Sunday, September 29, 2019

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI KAIRUKI KATIKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA UNGA WA MHOGO-CSTC LINDI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula wakisalimiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) walipotembelea kiwandani hapo kwa lengo la kukagua mazingira ya kiwanda hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake mkoani Lindi ili kusikiliza na kutatucha changamoto za wawekezaji.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula akijibu hoja za masuala ya ardhi kwa watendaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) kilichopo Wilaya ya Lindi Vijijini alipotembea mwishoni mwa wiki.Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (kushoto kake) pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (kulia kwake) kilichopo Lindi alipotembelea kiwandani hapo.Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile  akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo inayotumika katika kiwanda cha CSTC kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula kilichopo Lindi Vijijini alipotembelea kiwandani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) wakiangalia moja ya mfuko wa unga wa muhogo uliotengenezwa na kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akiuliza swali kwa Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile (wa kwanza kushoto mwenye kofia) wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Shaibu Ndemanga (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi na watumishi wa kiuwanda cha kutengeneza unga wa muhogo kilichopo Lindi.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment