Mkurugenzi Mtendaji MNH Prof.
Lawrence Museru akiongea na Maafisa Mawasiliano wa MNH, JKCI, MOI na
MUHAS (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi akiongea na Maafisa Mawasiliano wa MNH, JKCI, MOI na MUHAS
(hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu ya maafisa
mawasiliano
Baadhi ya Wakurugenzi MNH na
mawasiliano wa MNH, JKCI, MOI na MUHAS wakifuatilia mada wakati wa
ufunguzi wa mafunzo maalumu ya maafisa mawasiliano.
……………….
Maafisa Mawasiliano wa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba
Muhimbili (MUHAS), wametakiwa kutangaza maboresho makubwa ya uboreshaji
huduma za
afya yaliofanywa na Serikali ya awamu ya tano.
Wito huo umetolewa leo na Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akifungua mafunzo maalumu ya
utumiaji sahihi wa mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma kuhusu
taarifa mbalimbali katika taasisi hizo.
“Suala la kutoa habari kwa umma
kwa sasa si suala la kiutashi tena bali ni takwa la kisheria kwa mujibu
wa sheria ya huduma za habari pamoja na sheria ya haki ya upatikanaji
habari,” alisema Dkt. Abbasi
Aidha sekta ya afya imeboreshwa
sana tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani na maboresho
makubwa yamefanyika ikiwamo upatikanaji wa vipimo muhimu kama CT scan na
MRI pamoja na uhakika wa upatikanaji wa dawa katika Hospitali
mbalimbali nchini.
“Hivi karibuni nilitembelea
Muhimbili na nilijionea mageuzi makubwa yaliyofanyika, nimekutana na
wataalamu mbalimbali ambao wamenieleza mambo makubwa yanayoendelea hapa.
Sasa mambo haya yote ni vizuri maafisa mawasiliano muyasemee ili
wananchi waweze kuelewa,” alisema Dkt. Abbasi.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof.
Lawrence Museru amesema uongozi umeamua kuitisha mafunzo hayo kwa
watumishi wa kitengo cha habari na mawasiliano kwa kuwa hivi sasa kuna
mabadiliko makubwa katika sekta ya upashanaji habari hivyo ni lazima
wajifune mbinu mpya.
Mafunzo haya yamefunguliwa leo,
yatatolewa kwa siku nne na wakufunzi kutoka Ofisi ya Msemaji Mkuu wa
Serikali yanalenga kuwajengea uwezo watumishi wa Vitengo vya Habari na
Mawasiliano kutoka MNH, MOI, JKCI na MUHAS.
No comments:
Post a Comment