Mgeni
rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga (katikati) akiwa
ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo (kushoto), Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege
(kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi pamoja na
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari mara baada ya kuwasili
kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Mshehereshaji
ambaye pia ni mkufunzi wa Redio za Jamii, Rose Haji Mwalimu
akitambulisha meza kuu (haipo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Kutoka
kushoto meza kuu ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO
nchini, Nancy Kaizilege, Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo,
Mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga, Mwenyekiti
wa MISA Tanzania, Salome Kitomari pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TADIO,
Maimuna Msangi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji
Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli
mkoani Morogoro.
Mgeni
rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga akizungumza na
wadau wa tasnia ya habari na waandishi kutoka vyombo vya mbalimbali vya
habari jamii nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro
Hoteli mkoani Morogoro.
Mkuu
wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo akitoa salamu za Mkuu wa mkoa wa
Morogoro wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani
Morogoro.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege
akitoa salamu za UNESCO kwa niaba ya Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa
Shirika hilo nchini, Tirso Dos Santos (hayupo pichani) wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Mwenyekiti
wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi akitoa salamu za TADIO wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Mwenyekiti
wa MISA Tanzania, Salome Kitomari akizungumza wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Ofisa
habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNIC),
Didi Nafisa akiendesha majadiliano wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Baadhi
ya wadau wakongwe katika tasnia ya habari nchini wakiwasilisha maoni
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani
Morogoro.
Baadhi
ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Redio Jamii na wadau wa
tasnia ya habari nchini walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro
Hoteli mkoani Morogoro.
Mgeni
rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga na meza kuu katika
picha ya pamoja na Sekretarieti iliyofanikisha maandalizi ya
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Mgeni
rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Dk Augustine Mahiga na meza kuu katika
picha ya pamoja na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Redio Jamii
na wadau wa tasnia ya habari nchini walioshiriki maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Morogoro Hoteli mkoani Morogoro.
Maafisa
kutoka Umoja wa Mataifa Rose Mwalongo (wa pili kushoto) na Stella Vuzo
(wa pili kulia) katika picha ya kumbukumbu na wadau wa tasnia ya habari
nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morogoro Hoteli mkoani
Morogoro.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
SERIKALI
kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa taarifa imesema ipo tayari
kuangalia vikwazo vinavyosababisha ukosefu wa taarifa sahihi, ikiwamo
sheria ili uchakataji wa habari uboreke kwa manufaa ya taifa.
Aidha
imesema kwamba inatambua matatizo mengi duniani yanayosababisha uhasama
yanatokana na kukosekana taarifa sahihi miongoni mwa wanadamu.
Aidha
kukosekana kwa taarifa sahihi na kuwapo kwa taarifa za uongo
kumesababisha kuwapo kwa vita na usumbufu mwingine ambao ungeliweza
kutatuliwa kwa kuwapo kwa taarifa zilizo sahihi.
Kauli
hizo zimetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga
kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa
iliyoadhimishwa mkoani Morogoro hapa nchini yakiwa na kauli mbiu
“Upataji Taarifa : Asiachwe Mtu!”.
Alisema
ili taifa la Tanzania lisiingie katika migogoro serikali ipo tayari
kusikiliza wadau na kushirikiana nao kuweka mazingira ya upatikanaji wa
taarifa kuwa bora zaidi na unaojali maslahi mapana ya nchi.
Pamoja
na kuwapongeza waandazi wa hafla hiyo, UNESCO, Dk. Mahiga pia
alielezea umuhimu wa taasisi za umma na binafsi zinazohusika na upashaji
habari kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu na weledi mkubwa ili kuondoa
matatizo yanayoambatana na kukosekana kwa habari.
Alisema uchakataji wa habari ni muhimu ili wananchi wote waweze kupata habari na kuzitumia kwa maendeleo yao.
Alisema
suala la upatikanaji wa taarifa sahihi si wa taifa moja tu bali dunia
nzima na hilo limehimizwa tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia
ambayo kwa namna fulani ilichochewa na kukosekana kwa habari sahihi.
Alisema
pamoja na dunia mataifa kuridhia haki ya kujieleza na kupata habari,
mataifa na watu wengi wamekuwa wakikosa au wakinyimwa haki ya
kuhabarishwa na hivyo kuzua matatizo katika jamii husika.
Alisema
ndio maana Tanzania imekuwa moja ya nchi iliyotia saini mikataba uhuru
na haki ya kupata habari na kutamka wazi katika katiba yake kuhusu haki
za habari.
Alisema
kuna manufaa makubwa kwa watu kuwa huru katika kuhabarishana kama
kuongeza uelewa wa jamii katika masuala mbalimbali yakiwemo ya afya
uchumi na namna ya kuishi.
Hata
hivyo alisema taarifa zinapokuwa mbaya na zisizojenga husababisha
migogoro na migongano katika jamii na hivyo kuitaka jamii kuhakikisha
kwamba inapata taarifa sahihi na zenye kujenga jamii husika.
Alisema
kwa kuwa utawala bora unahusisha na demokrasia ni vyema kwa nchi yoyote
inayojinadi kuwa na demokrasia ni lazima kuwa na jukwaa kwa wananchi
wake kupata habari sahihi.
Waziri huyo alisema kwamba habari ni kama upanga wenye makali pande zote unaoweza kuleta neema au balaa .
“Habari
zikitumika vyema zinaleta haki na zikitumika vibaya zinaleta migogoro
na kuhatarisha usalama wa nchi“ alisema Dk. Mahiga.
Alipotolea
mfano wa uchaguzi wa serikali za mitaa na kusema kwamba ili wananchi
waweze kuufanya kwa ufanisi mkubwa ni lazima wawe wameelimishwa vya
kutosha kutambua na kujitambua ili wapige kura zenye uhakika.
Alipongeza
Mtandao wa Radio za Jamii (TADIO) kwa kuwa karibu na wananchi na kusema
wanafanyakazi njema ya kuhabarisha jamii hasa kutokana na ukweli kuwa
radio ya taifa haifiki kila mahali.
Alisema
kazi inayofanywa na TADIO ni ya muhimu kwani inasaidia serikali katika
kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na hasa mwelekeo
kama taifa.
Alisema
kutokana na ufanisi huo ni vyema taasisi hizo zikajikita katika kueleza
ukweli kwa weledi mkubwa ili wasiingie katika mtego wa kusumbuana na
sheria na hivyo kurejesha nyuma matunda muhimu ya haki za kupashana
habari.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi akizungumza kabla ya Waziri
Mahiga alishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kwa kuwezesha kuwepo kwa tukio hilo muhimu hapa
nchini.
Aidha
alishukuru kuwapo kwa makubaliano ya awali kati ya TADIO na Chuo Kikuu
Huria yaliyowezesha Mtandao huo wa Redio Jamii kuwa na ofisi katika
majengo ya chuo hicho.
Pia alishukuru UDOM kwa kuruhusu mifumo yake ya Tehama kutumika na kuja kuwa sehemu ya mafunzo kwa wanahabari.
Pia alishauri taasisi zote husika kuona changamoto zinazokabiliwa na redio jamii na kuzishughulikia.
Naye
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari akizungumza alisema kwamba
nchi zilizoendelea zimefanikiwa kutokana na kutumia vyema haki ya
upashanaji habari.
Alisema
hata hivyo hali bado si nzuri kwa upande wa watumishi wa umma ambao
wamekuwa wagumu kutoa taarifa mbalimbali zinazohitajika na vyombo vya
habari kwa ajili ya kufikisha kwa umma.
“ Kumekuwa na usiri mkubwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kuleta sintofahamu” alisema Kitomari.
Alitoa wito kwa watumishi wa umma kujengewa uwezo ili waweze kushiriki kikamilifu katika suala zima la uchakataji habari.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Nancy Kaizilege
alisema katika hotuba aliyosoma kwa niaba ya Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Tirso Dos Santos kwamba shirika hilo linaridhishwa na kasi ya
TADIO na kutaka wananchi kutambua haki zao za msingi za kupashana habari
na kufanya hivyo kwa weledi.
Mkuu
wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo akizungumza kwa niaba ya mkuu wa
mkoa alisisitiza umuhimu wa kutumia habari kuharakisha kasi ya
maendeleo.
TADIO
– Tanzania Development Information Organisation ni asasi ya habari za
maendeleo Tanzania inayohusisha vyombo vya habari za kieletroniki yaani
Radio zinazozalisha maudhui ya kijamii ambazo nyingi hupatikana mikoani
na sehemu za vijijini ambako idadi kubwa ya Watanzania wanaishi.
TADIO
ina jumla ya Radio wanachama 32 katika mikoa yote ya Tanzania bara na
visiwani isipokuwa Tabora na Singida. Uwezo wa Radio Jamii hizi kufikia
watanzania waliopo mikoani na hasa vijijini hukadiriwa kufikia asilimia
70%.
TADIO ilianzishwa rasmi mwaka 2017 baada ya kuvunjika kwa asasi ya mfanano ya awali iliyojulikana kama COMNETA
No comments:
Post a Comment