Wadau wa mazao ya nafaka, wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Japhate Hasunga wakati akihutubia mkutano wa siku mbili wa Wafanyabiashara
wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam
Mhe. Waziri Hasunga.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akihutubia mkutano huo.
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Bi.
Margareth Nzuki (katikati), akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF
akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na Dkt. Bunogelo
kuhusu utafiti ambao ulifanywa na Taasisi hiyo kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Mkuurgenzi Mtednaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw.Japhet Justine akipiga makofi wakati mkutano huo ukiendelea.
Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
Bi.Margareth
Nzuki (kushoto), kutoka ESRF akibadilishana mawazo na Bi. Vumilia L.
Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo wakati wa mkutano huo.
Mshiriki akitoa maoni yake.
Oswald
Mashindani (kushoto), kutoka ESRF akizunhumza jambo mbele ya Katibu
Mkuu (mstaafu) Wizxara ya Fedha, Bw. Paniel Lyimo (katikati) wakati wa
mkutano huo.
Mhe. Hadsunga (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na manaibu waziri makatibu wakuu na Mwenyekiti wa TPSF.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
|
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
MKUTANO
wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi
umefunguliwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
leo Agosti 29, 2019.
Mkutano
huo ambao umewajumuisha wasindikaji, wasafirishaji na wamiliki wa
maghala ya nafaka Lengo lake ni kuangalia fursa zilizopo kwenye tasnia
ya nafaka na jinsi ya kuzifikia ikiwa ni pamoja na masoko.
Akizungumza na washiriki wa mkutano huo uliowakutanisha
wadau kutoka mikoa mbalimbali nchini, Mhe. Hasunga ambaye alifuatana na Manaibu wake, Mhe. Husein Bashe, na Mhe.
Omary Mgumba alisema mkutano huo utatoa fursa kwa wajumbe kuelimishwa
kuhusu fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika, uwezo
wa Tanzania kuzalisha na nafasi ya wafanyabiashara kushiriki kikamilifu
lakini pia
washiriki watapata fursa ya kujifunza athari za upotevu wa mazao ya
nafaka baada yamavuno na mkakati wa serikali kudhibidi hali hiyo.
“Kitaalamu wanasema utafiti uliofanyika Tanzania na
nchi nyingi za Kusini asilimia 40 ya mazao yote yakiwemo ya
nafaka yanapotea baada ya mavuno kwa kuharibika na matatizo mengine, hii
haikubaliki mkulima amewekeza, amevuna halavu mazao yake yanaharibika,
lazima tuwe na mkakati wa kuzuia hali hii.” Alitoa hakikisho Mhe. Waziri
Hasunga na kuongeza.
Kulingana
na uzalishaji uliopo, nafaka nyingi kama mahindi mtama na nafaka
nyingine huhifadhiwa katika kiwango kisichoridhisha hali hii huchangia
kupoteza ubora wa nafaka na hatimaye huchangia kuzorota kwa ustawi wa
afya zetu, alifafanua zaidi Mheshimiwa Waziri.
Alisema
Agosti 1, mwaka huu kwenye sherehe za Nanenane kwenye viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganow a
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua mkakati wa namna ya
kupambana na kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno.
Katika utafiti wake ilioufanya hivi karibuni Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya Mradi wa Rapid Response Implementation Support to the Ministry of Agriculture and Agriculture Sector Lead Ministry (RARIS) unaofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation umebaini kuwa hali ya maghala mengi ya watu binafsi hayatoi taarifa serikalini na hii ni kutokana na mfumo wa sasa wa maghala.
Akitoa mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses),
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
Dkt.Hoseana Lunogelo alisema ESRF ilifanya utafiti wa hali (status) ya
maghala nchini na kubaini kuwa maghala ya watu binafsi hayalazimiki
kisheria kutoa taarifa serikalini kuhusu nini kimehifadhiwa na kiasi
gani cha nafaka
kilichohifadhiwa ndani ya maghala hayo na hali hii serikali inategemea tu maghala ya Serikali yaani (Public Storage
Facilities ) kupitia Werehouse Reseat Regulatory Board ili kujua takwimu za hali ya chakula nchini.
“Kwa
sasa kuna maghala 3,430 yaliyopo kati ya hayo ni 185 tu ndiyo kuna
uhakika wa kupata tawimu endapo zitahitajika lakini yaliyosalia huwezi
kupata takwimu hizo kwa sababu hakuna sheria inayowalazimisha kufanya
hivyo.” Alifafanua Dkt.
Lunogelo.
Alisema
hii ni changamoto kubwa, kama serikali inapata taarifa kutoka kwenye
maghala machache sana nchini na yale mengi haipati taarifa zake, maana
yake Serikali haiwezi kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na upatikanaji wa
chakula nchini na
hiyo ina athari mbaya kwenye usalama wa chakula na pia ina athari mbaya pia kwenye biashara.” Alsiema Dkt. Lunogelo.
|
No comments:
Post a Comment