Pages

Friday, August 30, 2019

SERIKALI KUJA NA MKAKATI WA MIAKA 5 MABORESHO YA SEKTA NDOGO MFUMO WA HAKI JINAI


Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga,akizungumza wakati wa kufungua kikao cha Mawaziri, Makatibu wakuu wa Wizara na wakuu wa taasisi zinazounda jukwaa la haki jinai ambao ulikuwa wa kujadili hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la majadiliano yaliyoanza Julai mwaka huu.

Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome,akizungumza katika kikao cha kujadili hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la majadiliano yaliyoanza Julai mwaka huu.
Kamishna wa polisi mstaafu Laurean Tibasana.akitoa taarifa katika kikao cha kujadili hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la majadiliano huo ambao ulianza Julai mwaka huu.
Sehemu ya wadau wakifatilia kikao cha kujadili hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la majadiliano huo ulioanza Julai mwaka huu.
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha Mawaziri, Makatibu wakuu wa Wizara na wakuu wa taasisi zinazounda jukwaa la haki jinai jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga,amesema kuwa Serikali inakuja na
mkakati wa miaka mitano utakaotekelezwa na Wizara na taasisi mbalimbali katika maeneo yanayohitaji mfumo wa maboresho ya haki jinai hapa nchini.
 
Dk.Mahiga ameyasema leo jijini Dodoma  wakati akifungua kikao cha Mawaziri, Makatibu wakuu wa Wizara na wakuu wa taasisi zinazounda jukwaa la haki jinai.
 
Mkutano huo wa kujadili hitimisho la mchakato wa sekta ndogo ya mfumo wa haki za jinai,zoezi la majadiliano likianza Julai mwaka huu.
 
Dk. Mahiga amesema kuwa  mara ya mwisho kupitia mfumo huo na kuufanyia maboresho ni takribani miaka 20 hivyo ni muhimu kupitia ili kuendana na wakati tuliona nao sasa.
 
Hata hivyo amesema  kuwa baada ya mapitio ya mfumo huo yatapitishwa na kujadili maeneo yaliyopendekezwa kuboreshwa ili kufanya mfumo huo kuwa Rafiki kwa wadau wote wa haki jinai.
 
” Niwapongeze wataalamu wetu ambao mmekua hapa kwa kwa kipindi cha  miezi miwili na wote ambao mmeshiriki katika kazi hii hadi hatua hii ya leo.
 
Dk.Mahiga amesema kuwa mfumo huo unahusisha mnyororo wa hatua mbalimbali zinazotolewa wakati wa kushughulikia uhalifu wa kuanzia katika ngazi ya kuzuia uhalifu kufuatilia mienendo yao wanapomaliza kutumikia adhabu.
 
Waziri amesisitiza zaidi  kuwa katika mnyonyoro huo mambo mbalimbali yamewekwa kisheria ya namna ya kushughulika na wahalifu ambayo yanashughulikiwa na Vyombo au taasisi za jukwaa la haki jinai hivyo lazima kufanya maboresho
Naye Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa kikao hiko ni muhimu sana kwa sababu kina lenga kufanya majadiliano ya hitimisho la mchakato wa maboresho ya sekta ndogo ya mfumo wa haki jinai.
Hata hivyo amesema kuwa ni vema nao wataalamu waliopo wanatumia nafasi hiyo kujadili maboresho hayo ili yalete tija na jamii kwa ujumla.
Prof.Mchome amesema kuwa kutokana na hilo wanapaswa kutumia nafasi hiyo kutekeleza kile kinachotakiwa ndani ya majadiliano hayo.
Naye Kamishna wa polisi mstaafu Laurean Tibasana amesema kuwa wanaipongeza serikali kutokana na jitihada inazofanya katika maboresho ya sekta ndogo ya sheria ya mfumo wa haki jinai.
Aidha amesema kuwa hilo litasaidia nchi kuwa na maendeleo kutokana na kwamba kutasaidia kupunguza uhalifu mbalimbali ikiwemo kurekebisha tabia  za wahalifu na kufuatilia mienendo yao wanapokuwa wamemaliza kutumikia adhabu walizopewa.

No comments:

Post a Comment