Pages

Friday, August 30, 2019

MAKAMISHNA WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WALIOSTAAFU UTUMISHI WAO KWA MUJIBU WA SHERIA, WAAGWA JIJINI DAR

Kamishna Mstaafu wa Magereza, Gedion Nkana(kushoto) na Kamishna Mstaafu wa Magereza, Augustine Mboje(kulia) wakiwa kwenye gari maalum wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam Agosti 30, 2019.
Makamishna Wastaafu wa Magereza wakipita katika gari maalum wakiwapungia mikono Maafisa na askari pamoja na Wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Agosti 30, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto) akiwa na Maafisa Waandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wakiwapungia mikono Makamishna Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Agosti 30, 2019.
Kamishna Mstaafu wa Magereza, Gedion Nkana akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo leo Agosti 30, 2019.
Gwaride maalum lililoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza likipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Makamishna Wastaafu wa Jeshi hilo ambao wamestaafu utumishi wao kwa mujibu wa Sheria.
Kamishna Mstaafu wa Magereza, Gedion Nkana(kushoto) na Kamishna Mstaafu wa Magereza, Augustine Mboje(kulia) wakiwa katika jukwaa kuu wakipokea salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride maalum la kuwaaga leo Agosti 30, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, John Casmir Minja mara baada ya gwaride maalum la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Jeshi hilo ambao wamestaafu utumishi wao Jeshini kwa mujibu wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Jenerali Wastaafu wa Jeshi la Magereza(walioketi) pamoja na Makamishna Waliopo wa Jeshi Magereza, Makamishna Wastaafu wa Magereza na Maafisa Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya ya Gwaride rasmi la kuwaaga Makamishna Wastaafu wa Jeshi hilo leo Agosti 30, 2019(Picha zote na Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment