Washiriki
wa mafunzo ya kupinga mila potofu ya ukeketaji wakionesha mshikamano wa
mapambano dhidi ya vitendo hivyo baada ya kuunda kamati za ulinzi wa
mama na mtoto katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida juzi.
Mwezeshaji
wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu, Japhet Kalegeya akizungumza
katika mkutano wa kuunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto wilayani
Ikungi mkoani humo.
Afisa
Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi, Haroon Haroon akiwasilisha mwongozo
wa ( MTAKUWA) kwa kamati za ulinzi wa mama na mototo ngazi ya Kata sita
za Ikungi,Ihanja, Iglanson, Iseke, Mhintiri na Minyughe.
Mwezeshaji, Daniel Saido akiwa na Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo katika mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Ihanja, Sombi Majuta akizungumza katika mkutano
Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo akizungumza katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHIRIKA
la Foundation for Civil Society (FCS) limetoa shilingi milioni 40 kwa
ajili ya mradi wa kupambana na mila potofu za ukeketaji mkoani Singida
ambao umeanza mwezi Julai hadi Machi 2020.
Fedha
hizo zimetolewa kwa Shirika lisilo la kiserikali la Save the Mother and
the Children of Central Tanzania (SMCCT), ambalo limeunda kamati za
ulinzi wa mama na mtoto kwenye kata sita na vijiji 18 katika Wilaya ya
Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya mapambano hayo.
Imeelezwa kwamba majukumu ya kamati hizo ni kumlinda mama na mtoto dhidi ya vitendo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia.
Hayo
yalisemwa na mwezeshaji wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu,
Japhet Kalegeya wilaya ni hapa juzi wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mradi huo ambao utasaidi kupunguza vitendo hivyo au
kuvimaliza kabisa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.
Alisema
wamefikia uamuzi wa kuanzisha kamati hizo ili ziweze kuharakisha
kutokomeza kabisa vitendo hivyo ambavyo vipo kinyume na haki za binadamu
kama vile ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba za utotoni, ndoa
za utotoni ,ubakaji ,ulawiti,ukeketaji na udhalilishaji wa kijinsia
katika wilaya hiyo.
“Mradi
huu wa utetezi dhidi ya mila potofu ikiwemo ukeketaji na ukatili wa
kijinsia unalenga kuwafikia wanawake na wasichana wapatao 7,200 katika
wilaya ya Ikungi ambapo hali ya unyanyasaji wa kijinsia ni mbaya”,
alisema Kalegeya.
Akitolea
mfano wa hali hiyo alisema kuanzia Januari hadi oktoba 2018 jumla ya
wanafunzi 23 waliokuwa kati ya kidato cha kwanza na nne walipachikwa
mimba wilayani Ikungi.
Naye
mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Masinda, Rosemary
Seith, amelishukru na kulipongeza shirika la SMCCT kwa kushirikisha
baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwapa elimu juu ya
madhara ya ukeketaji na ukatili wa kijinsia.
“Sisi
tuliohudhuria mafunzo haya yametusaidia kujua kwa mapana madhara ya
vitendo hivyo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia sasa tunaenda
kuwaelimisha na wenzetu ambao hawakubahatika kupata mafunzo haya hapa
leo”, alisema.
Mratibu
wa mradi huo, Evaline Lyimo, ametaja baadhi ya malengo ya mradi huo
kuwa ni kuongezeka kwa uelewa kwa jamii kuhusu kudhibiti vitendo vya
ukatili wa kijinsia na ukeketaji na kuimarisha mfumo wa utoaji wa
taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii hadi ifikapo
Machi mwaka 2021.
Kata zilizounda kamati hizo ni lkungi, Ihanja, Iglansoni,Iseke, Minyughe na Muhintiri.
No comments:
Post a Comment