Pages

Friday, August 30, 2019

SERIKALI YAFUTA MILIKI YA MASHAMBA YA MOA MKINGA


 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga Dustan Kitandula alipokwenda kutangaza uamuzi wa Serikali kufuta Mashamba matatu ya Mkomazi Plantantions Co Ltd maarufu kama MOA leo tarehe 30 Agosti 2019.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mayomboni kilichopo wilaya ya Mkinga mkoani Tanga alipokwenda kutangaza uamuzi wa Serikali kufuta Mashamba matatu ya Mkomazi Plantantions Co Ltd maarufu kama MOA leo tarehe 30 Agosti 2019.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mayomboni kilichopo wilaya ya Mkinga mkoani Tanga alipokwenda kutangaza uamuzi wa Serikali kufuta Mashamba matatu ya Mkomazi Plantantions Co Ltd maarufu kama MOA leo tarehe 30 Agosti 2019. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga Dustan Kitandula.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Dustan Kitandula (kushoto) alipokwenda kutangaza uamuzi wa Serikali kufuta Mashamba matatu ya Mkomazi Plantantions Co Ltd maarufu MOA leo tarehe 30 Agosti 2019. 
 (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)Na Munir Shemweta, MKINGA
Serikali imefuta miliki ya Mashamba matatu ya Mkomazi Plantantions maarufu MOA yaliyopo wilaya ya Mkinga mkoani Tanga kutokana na kukiuka masharti ya uendelezaji ikiwemo kutelekezwa bila kufanyiwa maendelezo yaliyokusudiwa  na kutolipiwa kodi ya pango la ardhi.
Uamuzi huo umetangazwa leo tarehe 30 Agosti 2019 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipozungumza na wananchi wa Mayomboni wilayani Mkinga mkoani Tanga alipokwenda kutatua mgogoro wa muda mrefu katika eneo hilo.
Mashamba yaliyofutiwa ni lenye hati Na 9780  na ukubwa wa ekari 14,688, shamba  Na 4268  ekari 804 na Shamba lenye Hati Na 9781  ekari 246 ambapo mashamba yote matatu yana ukubwa wa ekari 15,738.
Kufuatia uamuzi huo, jumla ya vijiji kumi vyenye kaya 3,236 zilizo na wakazi 16,450 zitanufaika na uamuzi wa serikali kutokana na wananchi wake kuvamia mashamba hayo na kufanya maendelezo ya kujenga makazi, shule pamoja na kuendesha shughuli za kilimo cha mazao ya kudumu na ya muda mfupi.
Vijiji vilivyonufaika ni uamuzi wa Serikali kufuta mashamba ya Mkomazi Plantations ni kijiji cha Kilulu-Dunga, Zingibari, Mwaboza, Mwakikoya, Mhandakini, Nkanyeni, Sigaya, Mayomboni, Ndumbani pamona na kijiji cha Moa
Akizugumza wakati wa kutangaza uamuzi huo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema uamuzi wa kufuta mashamba hayo matatu unafuatia maombi yaliyotumwa kwa Raisi John Pombe Magufuli ya kutaka kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa na wamiliki wake kwa muda mrefu.
Alisema, Rais ameridhia maombi hayo kwa kuwa serikali imekuwa ikisisitiza utekelezwaji wa sheria ya Ardhi Na 4 ya mwaka 1999 ikiwemo uendelezaji wa mashamba ambayo yamemilikishwa sehemu mbalimbali nchini.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza kufanyika upimaji katika vijiji vyote kumi vilivyopo ndani ya shamba hilo sambamba na kuanishwa miapaka ya vijiji hivyo na kupatiwa hati ambapo alitaka wananchi wanaishi kwenye vijiji hivyo kutobughudhiwa.
Aidha, Waziri Lukuvi alitaka maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya uwekezaji katika shamba yaliyofutwa kuachwa kwa ajili ya shughuli hiyo ikiwemo muwekezaji wa Katani Azka International Tanzania mwenye ekari mia tano pamoja na maeneo ya viwanda kama kile cha kuzalisha chumvi na kusisitiza kuwa serikali inataka uwekezaji utakaotoa ajira kwa vijana na wakati huo kupata mapato kupitia kodi ya pango la ardhi.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameagiza kufanyika uhakiki wa mashamba mengine ya Kwa Mtili Estates Co Ltd yaliyopo Mkinga mkoani Tanga ambapo ekari 58 pekee ndizo zilizoombwa kufutwa kwa Rais kutokana na kutoendelezwa huku mmili wake ikidaiwa kumiliki ekari  2,841.
Hatua hiyo inafuatia Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika halmashauri ya wilaya ya Mkainga Obed Katonge kueleza kuwa, Kwa Mtili Estates Co Ltd inalo shamba la lenye ukubwa wa ekari 2,841 tofauti na inavyoonekana katika kumbukumbu za ofisi ya Msajili wa Hati Kanda ya Kaskazini ambazo ni 58.
Lukuvi aliagiza wataalamu wa ardhi kutoka Kanda ya Kaskazini kufanya uhakiki huo katika kipindi cha mwezi mmoja na kumpa taarifa ya uhakiki huo mwisho wa mwezi Septemba 2019 na kufafanua kuwa pale itakapothibitika kuna ujannja uliofanyika wa kumuongeza mmiliki wa shamba hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Mbunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga Dustan Kitandula aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kusikiliza kilio cha muda mrefu cha wananchi wanaoishi eneo la shamba lililofutwa la kutaka kurejeshewa ardhi yao waliyokuwa wakiutumia kwa shughuli mbalimbali.
Alisema, mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mkinga na wamiliki wa mashamba ya Mkomazi Plantantions Co Ltd umekaa kwa muda mrefu na kuwafanya wananchi kuwa na ndoto isiyokuwa na majibu lakini uamuzi uliotolewa na Serikali umewafanya kuishi kwa furaha na amani .

No comments:

Post a Comment