Mufti
wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally na Mh. Ali Davutoglu,
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wageni
wakibadilishana mawazo kabla ya kufuturu.
Muda wa Kufuturu (Iftar)
Maulid Kitenge (MC) akifurahia jambo pamoja na Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir.
Mufti
akitoa mawaidha kwa watu mbalimbali waliofika Kibada Gardens kwa ajili
ya Iftar maalum iliyoandaliwa siku hiyo,Mufti amewataka Waislamu
waendelee kumcha Mungu na kuendelea kufanya matendo mema yanayompendeza
Mwenyezi Mungu,na kwa si kwa wakati huu tu wa mwezi Mtukufu wa
Ramadhani,lakini pia wakati wote.
Sheikh wa msikiti wa Kibada akikabidhiwa baadhi ya vitu kwa ajili ya Futari kwa wakazi wa Kibada.
Balozi
wa Uturuki nchini Tanzania, Mr. Ali Davutoglu akipeana mkono na Sheikh
wa wilaya ya Kigamboni, Mr. Sharrif Hassan wakati wa Iftar iliyoandaliwa
na Kibada Gardens Dar es Salaam. Pili kushoto ni Sheikh Mkuu wa
Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir bin Ally
Sheikh
Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir bin Ally akitoa maneno ya
hekima kwa baadhi ya watu waliofika katika Iftar maalum iliyoandaliwa na
Kibada Gardens, Kigamboni Dar es salaam.
Mufti
wa Tanzania pamoja na baadhi ya masheikh wa bakwata wakiwasili Kibada
Gardens kwa ajili ya Iftar iliyoandaliwa maalum katika mfungo wa
Ramadhan unaoendelea.
Kibada
Gardens imeandaa Iftar maalum ambayo ilihudhuriwa na Mh. Mufti wa
Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally na Mh. Ali Davutoglu, Balozi
wa Uturuki nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment