Bw. Deonald Dea |
Na Vero Ignatus Arusha.
CHAMA
cha Wanasheria wa Afrika (PALU) kwa kuahirikiana na Taasisi zingine
ikiwemo inayosimamia matumizi ya kidijitali Duniani Article 19,
wamekutana Jijini Arusha kwa ajili ya kujadili na kuweka mikakati ya
kusimamia haki za watumiaji wa mitandao ya teknolojia ya kidijitali, ili
kuwezesha wananchi wa nchi hizo kupata huduma.
Bw. Deonald Dea ni Afisa mtendaji mkuu wa chama PALU ambapo
amesema kuwa, binadamu wana haki ya kupata huduma ya mawasiliano ya
kidijitali ili waweze kuendesha shughuli za kibinadamu vizuri.
Bw.Deya
alishauri badala ya serikali kukimbilia kufunga mitandao hiyo,
wangeiachia Bunge lipitishe sheria nzuri za kusimamia suala hilo na
huku Mahakama zikihakikisha zinapewa nafasi za kuhakikisha sheria hizo
zinasimamiwa na anayekiuka anapata stahiki yake
Bw. Dea
amesema kuwa Mawasiliano ni muhimu kwa wakati kama huu sababu mitandao
inatumika katika kufanya biashara ,kutoa elimu na hata maswala ya Afya
pamoja na mengine mengi.
"Sisi
kama binadamu tuna uhuru wa kuzungumza na uhuru wa kupata taarifa
sahihi na kwa mfumo wa sasa wa kutumia mawasiliano ya kidijitali kama
Intenet ndio njia kubwa za kusambaza habari na hapo kuna sheria
zinazotakiwa kuwepo ili kulinda uhuru huu kwa binadamu,”alisema"
Amesema
wamekutana wanasheria, wanaharakati, toka nchi za EAC na Maofisa wa
haki za binadamu wa jumuiya ya Afrika ya mashariki na Tume ya umoja wa
Afrika ya kupambana na Rushwa ,na Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu
na kijamii .
"Kwani
kweli hata serikali inatumia mitandao hii kufanikisha kukamata wahalifu
wa makosa mbalimbali , hivyo vema kila upande ukaheshimu haki ya
wengine na sio kukimbilia kuzuia wngine wasipate haki ya
mawasiliano,”alisema
Amesema
kuwa pamoja na haki hizo bado zipo baadhi ya serikali ya nchi hizo
zinakiuka haki za binadamu za uhuru wa kuhakikisha wanapata mawasiliano
kwa kufunga mitandaobya kijamii wakihofia kukashifiwa jambo balo siyo
sahihi
Ephraim
Kenyanito kutoka Afisa mipango wa kidigitali kutka Article 19 ya nchini
Kenya kuwa ni vyema kukawepo na sheria zitakazowasaidia wananchi
kutumia vizuri teknoloji kuweza kupata mawasiliano ya haraka na kufanya
biashara.“Hadi
sasa hatuwezi kuzifikia nchi zilizoendelea katika matumizi ya
kidijitali kwenye masuala mbalimbali , hivyo vema na nchi zetu za EAC
tukafanya jitihada kuweka mipango madhubuti ya kusimamia hili na
kueneza huduma hizo za mtandao kwa wananchi wote wa nchi za EAC, na
hasa vijijini,”alisema Mwisho.
Amesema
hivi sasa katika nchi nyingi wanawake wananwake hawajaunganishwa
kutumia teknolojiankama wanaume hivyo watafiti watumie sheria jinsi ya
kufanya ili watu watumie mitandao.
No comments:
Post a Comment