Na Ahmed Mahmoud,Arusha.
Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga
amefungua mkutano mkuu wa wanahisa wa Chama cha Wakulima la Tanganyika
(TFA) kilichowakutanisha wadau wa kilimo na wanahisa kwa
pamoja ili
kujadili maendeleo ya kilimo.
Hasunga ameipongeza TFA kwa juhudi
wanazozifanya katika kukuza sekta ya kilimo nchini ambayo ni kiinua
mgongo na imeajiri watu wengi zaidi ya asilimia 80% ya Watanzania.
Akizungumza katika mkutano huo ambao uliambatana na utoaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wakulima hao .
Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na TFA katika kutatua changamoto za wakulima ili kuboresha sekta ya kilimo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima
TFA Peter Sirikwa amesema kuwa TFA iko mstari wa mbele katika
kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini na kuwanganisha wadau wa kilimo
kwa pamoja .
No comments:
Post a Comment