Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akifungua kikao
cha Vyama vya Siasa kupitia na kujadili Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa Mwaka 2019.
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya
Siasa, John Shibuda akizungumza wakati wa Kikao cha kujadili rasimu ya
kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019.
Baadhi wa wajumbe wakifuatilia ufunguzi wa kikao cha kujadili rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.
Selemani Jafo (Katikati) akiwa katika picha ya mpamoja naMwenyekiti wa
Baraza la Vyama vya Siasa pamoja na viongozi wengine wa vyama vya siasa
vilivyoshiriki katika kikao.
…………………………..
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo wamewataka viongozi
na wawakilishi vya vyama vya siasa kuhakikisha wanatoa maoni yenye
tija
ili kutengeneza kanuni zilizo bora zitakazo simamia uchaguzi wa serikali
za mitaa.
Aidha, Jafo amesema uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika muda wote kati ya Novemba au Desemba mwaka huu.
Jafo aliyasema hayo wakati wa
kufungua mkutano wa siku mbili uliokutanisha vyama vya siasa vyenye
usajili wa kudumu ambao wana kazi ya kujadili rasimu ya uchaguzi wa
serikali za mitaa unaofanyika baadaye mwaka huu.
Alisema Tanzania inaongozwa kwa
utaratibu wa demokrasia, hivyo Serikali ilioana kutengeneza jukwaa la
kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo vyama vya saisa ili kuwa na
kanuni bora zitakazoendesha uchaguzi kwa amani na utulivu.
“ Nikiwa nimepewa mamlaka hii na
Rais John Magufuli, nikaona sio vyema kwa mujibu wa utaratibu wa undwaji
wa kanuni hizi lazima tuunde kanuni ambazo zinamchango mkubwa wa wadau
mbalimbali ambao utasaidia sana katika mwenendo wa uchaguzi tunaoendana
nao
“Tunapokea maoni kutoka kwa wadau,
na kundi hili ambalo linawakilisha vyama vya siasa vyenye usajili ni
muhimu sana kwasababu ndio kundi ambalo linachakata kwa muda wote katuni
hizi na wenye wajibu wa kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali.
Alisema kutokana na umuhimu wa
vyama vya siasa katika uundwaji wa kanuni za uchaguzi, ofisi yake
ilipeleka rasimu hiyo mapema kwa wadau ili kuweza kupata muda wa kupitia
na kuja na maoni yaliyobora.
“Ndio maana nimewapa maelekezo ni
vyema kanuni kuwafikia wadau siku chache kabla hatujakutana wapate muda
wa kuzipitia ili kupata maoni mazuri.
Aliongeza: “ Wakati mwingine
tukipeana kanuni ukumbini, inakuwa sio jambo jema sana na inakuwa kama
ni jambo la kuviziana, hili ni jambo letu sote kwa ajili ya nchi yetu,
mapema kupata ushauri mzuri ulio bora na kanuni ziwe nzuri na imara ili
kuweza kushiriki uchaguzi za serikali za mitaa kwa uzuri.
Jafo alisema kanuni hizo
zinamaeneo matatu ikiwa ni pamoja na Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa
mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa halmashauri ya kijiji na mwenyekiti wa
kitongoji katika mamlaka ya serikali za mitaa za mwaka 2019.
Alisema pia kuna Rasimu ya
uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa, na wajumbe wa kamati ya mtaa katika
mamlaka ya miji za mwaka 2019 na Rasimu ya kanuni ya uchaguzi wa
mwenyekiti wa kitongozi katika mamlaka za miji midogo za mwaka 2019.
“ Nimatumiani yangu tutatumia muda
vizuri katika kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni na michango
mbalimbali kusaidia kuboresha rasimu za kanuni kwa lengo la kukuza
demokrasia hapa nchini na utawala bora.
“ Taifa letu ni taifa la mfano,
pengine mataifa mengine hayapati jukwaa kama hii la kuweza kubadilishana
mawazo hivyo kuzidi kuimarisha demokrasia,” alisema.
Aliongeza: “ Ni imani yangu
mchakato utaenda vizuri na utakuwa wenye tija kwa wajumbe kutoa maoni
bora ili mwisho wa siku shiriki Novemba au mwishoni wa mwaka huu kwa
jinsi Mungu atakapotupa kibari.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la vyama
vya Siasa, John Shibuda alisema watahakikisha wanatengeneza kanuni
zitakazojenga taswira nzuri ya nchi Kitaifa na Kimataifa.
Aliomba katika kikao hicho Msajili
wa vyama atoe uwianishaji wa kanuni hizo pamoja na Sheria mpya ya vyama
vya siasa ili isijeleta msuguano wakati wa uchaguzi huo.
“Ili kuondokana na dukuduku na
sintofahamu kuwepo uwianishaji wa sheria ya vyama vya siasa na kanuni
hizi za uchaguzi, tuongeze muda wa majadiliano uwe siku tatu ili
tumsikie msajili anasemaje kwenye hili ili isitokee misuguano,”alisema.
Pia Shibuda alipongeza juhudi za
Rais John Magufuli za kuimarisha uchumi wa nchini na kuwa wao kama vyama
siasa hawana upogu wa macho na akili wa kutambua juhudi hizo.
Jana wajumbe walipitishwa katika
rasimu hiyo na watatumia siku ya leo kufanya majadiliano na kesho
itakuwa zamu ya asasi za kiraia kutoa maoni yake.
Baadhi ya vyama vilivyotuma
wawakilishi ni Chama cha Mapinduzi(CCM), Chama cha Wananchi(CUF), Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ARA, Union for Multiparty
Democracy(UMD), ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, National League For
Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party(UPDP), National
Reconstruction Alliance(NRA) na Tanzania Democratic Alliance(TADEA).
Tanzania Labour Party(TLP), United
Democratic Party(UDP), Demokrasia Makini (MAKINI), Democratic
Party(DP), Sauti ya Umma(SAU), Tanzania Farmers Party(AFP), Chama cha
Kijamii(CCK), Alliance for Democratic Change(ADC) na Chama cha Ukombozi
wa Umma(CHAUMMA).
No comments:
Post a Comment