Msimamizi
wa Usalama wa Waandishi wa Habari wa Wizara ya Habari, Utamaduni ,
Sanaa na Michezo, Patrick Kipangula akitoa neno la ufunguzi wakati wa
kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi
wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos akizungumza wakati wa
kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi
wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Ofisa
programu wa Unesco kitengo cha Habari na Mawasiliano, Nancy Kaizilege
akifafanua jambo wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali
kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Wadau
wa tasnia ya habari wakitoa maoni wakati wa kongamano la uandazi wa
taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika
mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini
Dar es Salaam.
Ofisa
programu wa Unesco kitengo cha Habari na Mawasiliano, Nancy Kaizilege
akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wadau wakati wa kongamano la
uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari
lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Unesco jijini Dar es Salaam.
wadau
wa tasnia ya habari walioshiriki kongamano la uandazi wa taarifa ya
serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni
mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es
Salaam.
Wadau
wa tasnia ya habari wakiendelea kujadiliana wakati wa kongamano la
uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari
lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Unesco jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos akifafanua jambo wakati
wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa
waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
SERIKALI
imesema kwamba iko tayari kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine kuhakikisha
usalama wa waandishi wa habari wakati wakitekeleza kazi zao.
Kauli
hiyo imetolewa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo wakati wa
kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi
wa habari.
Akizungumza
kwa niaba ya wizara Msimamizi wa Usalama wa Waandishi wa Habari,
Patrick Kipangula alisema kwamba serikali imeweka mazingira sawa ya
kumlinda mwandishi wa habari ili kuiwezesha nchi na wananchi kuwa na
taarifa za uhakika zinazogusa maisha na maendeleo yao.
Alisema
kwamba katika kongamano hilo ni vyema washiriki wake wote wakatazama
rasimu hiyo ambayo itakuja kuwasilishwa katika kikao kikubwa cha kitaifa
kuzungumzia usalama wa waandishi.
Akizungumzia
masuala ya sasa ambapo kukitokea tatizo kuhusu waandishi kunakuwa na
malalamiko mengi, alisema kwamba ni vyema ikatambulika kwamba sehemu
nyingi duniani na hapa nchini matatizo mengi dhidi ya waandishi wa
habari hayasababishwi na serikali bali na watu binafsi.
Alisema waandishi wanapaswa kuelewa sheria wanazofanyia kazi ili kujua haki zao na pia kujua misngi ya usalama wao.
Alisema
ni matumaini yake kwamba taarifa hiyo inayopikwa itasaidia kutambua
mazingira ya waandishi hapa nchini na kuwezesha kuwa na usalama zaidi
kama Umoja wa Mataifa unavyotaka katika kuzingatia vipengele vyake vya
maendeleo endelevu hasa kipengele cha 16 na 10 hasa kifungu cha kwanza
na cha pili kinachogusa usalama waandishi wa habari na wafanyakazi wa
habari.
Alisema
kwa sasa serikali imepania kuhakikisha kwamba waandishi wa habari
wanakuwa salama na kwamba uhuru wa habari hautishiwi kwa kuwanyima uhuru
waandishi wa habari.
Alisema
sheria ya vyombo vya habari imetengenezwa kumlinda mwandishi wa habari
hasa kwa kuzingatia kwamba waandishi pia wanatakiwa kupelekwa mafunzo na
kuwekewa bima.
Katika
mkutano huo ambao wawakilishi wa UNESCO walikuwepo, Mkuu wa Ofisi na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos aliwataka washiriki kuchangia ripoti
hiyo ili iweze kuwa msingi wa usalama kwa waandishi wa habari.
Alisema
taarifa hiyo ambayo pia imetengenezwa kwa taarifa kutoka katika
mashirika ya kiraia ni muhimu sana katika utekelezaji wa malengo
endelevu ya dunia.
Alisema
amefurahishwa sana na juhudi za serikali za kuandika taarifa hiyo, huku
akisema mchango wa wadau ni muhimu ili kuwa na ripoti iliyokamilika.
Hii
ni mara ya kwanza kwa serikali kuandaa ripoti kwa kusaidiwa na UNESCO
kuhusu usalama wa waandishi wa habari ingawa mashirika yasiyo ya
kiserikali yamekuwa yakifanya.
Ripoti
hiyo ya serikali inatarajiwa kuwasilishwa kwa mamlaka za juu na
kujadiliwa Juni mwaka huu, huku taarifa hiyo ikitakiwa kukamilika Mei.
Naye
Ofisa programu wa Unesco kitengo cha Habari na Mawasiliano, Nancy
Kaizilege alisema katika mkutano huo kwamba ripoti hiyo ni mchanganyiko
wa ripoti mbalimbali ikiwamo maswali yaliyoulizwa kwa kupitia mitandao.
Alisema kwamba taarifa hiyo inatarajiwa kufikishwa Wizara ya Fedha kabla ya kwenda kwenye mkutano mkubwa wa wadau.
Alisema kimataifa shauri hilo litakuwa wazi Julai mwaka huu wakati kwa Afrika itakuwa ni juni nchini Morocco.
Katika
mkutano huo uliofanyika katika ofisi za UNESCO, wadau walikuwa
wanaangalia rasimu ya serikali na usahihi wake kabla ya kwenda kwenye
majadiliano katika jukwaa kubwa la kisiasa baadae mwaka huu.
Kwa
mujibu wa vipengele vya SDG mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa
wanatakiwa kutoa taarifa za hiari kuhusu usalama wa waandishi wa habari
na wafanyakazi wa vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment