Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba
John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Libya
Mhe. Jamal El Barak
=======================================
Tanzania
na Serikali ya Umoja ya Libya, zimekubaliana kuingia katika mazungumzo
ya kina yenye lengo la kupitia miradi yote na uwekezaji, iliyokuwa
ikifanywa na Serikali ya Libya hapa nchini kabla ya machafuko nchini
humo na pia kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji ambayo Libya imeonesha
nia ya kutaka kuwekeza chini ya Kamati ya pamoja baina ya nchi hizo
mbili.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba
John Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa mazungumzo na
Kiongozi wa Ujumbe kutoka Libya na kuongeza kuwa baada ya hali ya Libya
kutengemaa na Amani kuongezeka wamekubaliana kuingia katika uwekezaji.
“Nimemueleza
mgeni wangu kuwa mwaka huu wa 2019 Tanzania tumeutangaza kuwa ni mwaka
wa uwekezaji na yeye ameonesha nia ya nchi yake na makampuni ya Libya
kutaka kuja kuwekeza hapa nchini,tumejadili pia jinsi ya kufufua kamati
ya pamoja kati ya Libya na Tanzania kwakuwa mkutano wa mwisho ulifanyika
mwaka 2000 baada ya Kamati hiyo kukutana sasa tutajadili miradi
mbalimbali ambayo Libya imewekeza,mitaji iliyoiwekeza lakini pia
tutaangalia maeneo mapya wanayopendekeza kuwekeza”
Aidha
Profesa Palamagamba John Kabudi amefafanua kuwa lengo jipya katika
sheria za uwekezaji Tazania ni kuhakikishia Nchi inakuwa na mfumo wa
sheria na uwekezaji ambao kila upande unapata tofauti na mfumo wa zamani
ambao wawekezaji walikuwa wakinufaika na nchi inanyonywa.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Ujumbe kutoka Libya Mhe. Jamal El Barak amesema
wamekuja dhumuni la ujumbe wao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ni kumjulisha kuwa Serikali ya Umoja wa
Libya iko tayari kufufua na kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia baina
ya nchi hizo baada ya hali ya Amani kutengemaa nchini Libya kutokana na
mahusiano ya Tanzania na Libya kuwa ya kihistoria.
Mbali
na hayo Mhe Jamal El Barak ameongeza kuwa Libya iko tayari kushirikiana
na Tanzania katika sekta mbalimbali za uwekezaji kwa kuwa wanatambaua
mazingira ya uwekezaji Tanzania ni mazuri hasa baada ya kuhakikishiwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuwa
mazingira ya uwekezaji yameboreshwa.
“Si
mara yetu ya kwanza kuwekeza hapa nchini,kabala ya machafuko nchini
mwetu tulikuwa tumewekeza katika sekta mbalimbali na sasa tutaangalia
maeneo mapya ya uwekezaji”
|
No comments:
Post a Comment