Waziri Mkuu mstaafu Edward
Lowassa akisalimiana kwa furaha na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip
Mangula pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili
katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akishuhudia.
Waziri Mkuu mstaafu Edward
Lowassa akitangaza rasmi kurejea chama cha Mapinduzi CCM mbele ya
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula, Katibu wa CCM Bashiru
Ally, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamojan na Kada wa CCM Rostam Azizi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa
ambaye amerejea rasmi CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo katika mazungumzo
na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, Kada wa CCM Rostam Azizi, Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula
pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment