Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya
Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama
kwenye ziara ya kikazi. (Picha na Ofisi ya Makamu Rais)
Matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu
ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika
miji ya Kagongwa na Isaka . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua matanki mawili ya maji
ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria
kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni
24.72. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Kagongwa,
wilayani Kahama waliojitokeza kwa wingi kumsalimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Kagongwa,
wilayani Kahama waliojitokeza kwa wingi kumsalimu. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira
yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka
kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen.(Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari NYASHIMBI
wakicheza ngoma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye aliweka jiwe la
msingi la ufunguzi wa madarasa la mradi wa TEA na P4R. Mkamu wa Rais
yupo wilayani Kahama kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua
shughuli za maendeleo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1, Machi 2019 ameendelea na
ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika
wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Akiwa Wilayani Kahama Makamu wa Rais
alitembelea mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya Ziwa Victoria kwennda
katika miji ya Kagongwa na Isaka wenye gharama ya shilingi bilioni
24.72 zikiwa fedha za ndani.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Isagehe ambapo pamejengwa matanki mawili ya maji ambayo yana uwezo wa
kubeba lita laki 8 kila moja, Makamu wa Rais alisema “Serikali ya awamu
ya tano inawajali na kuwathamini wananchi wake na kuwahakikishia
wananchi hao maji yatafika kote yalipoahidiwa”
Makamu wa Rais pia alitembea mgodi wa
dhahabu wa Buzwagi na kutaka kufahamu mgodi huo umejiandaaje kuyaacha
mazingira salama mara baada ya kufungwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri Madini
Mhe. Stanslaus Nyongo amesema sheria mpya ya madini itasaidia sana
katika kuboresha maisha ya Watanzania wengi kwani pamoja na kodi
itakayolipwa pia wachimbaji wanajukumu la kuchangia huduma za kijamii
kwenye maendeo yanayozunguka mgodi.
Aidha, Makamu wa Rais aliweka jiwe la
msingi la ufunguzi wa madarasa 8 ambao ujenzi wake umegharimu zaidi ya
shilingi milioni 121 ikiwa ni miradi ya TEA na P4R katika shule ya
Sekondari Nyashimbi wilayani Kahama.
Mwisho Makamu wa Rais alihutubia
wananchi wa Kahama katika uwanja wa michezo wa Taifa ambapo alihimiza
wananchi hao kushirikiana na Serikali katika masaula ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment