Mwili wa Mkurugenzi wa Vipindi
na Uzalishaji Clouds Media Group, Ndugu Ruge Mutahaba umewasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukitokea Afrika Kusini
alikokuwa akipatiwa matibabu.
Aliyeongoza mapokezi ya Mwili
wa Ruge Mutahaba ni Waziri January Makamba akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es aalaam Paul Makonda pamoja na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bw.
Joseph Kusaga.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Ruge Mutahaba likiwa linaondoka Airport kuelekea hospitali ya Lugalo.
No comments:
Post a Comment