NA OWM, RUVUMA
WAZIRI Mkuu,
Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uhakikishe kuwa vijana
wote wanaomaliza darasa la saba kwenye kila Halmashuri za mkoa huo
wanakwenda kuanza kidato cha kwanza.
Aametoa agizo hilo leo
(Jumatano, Januari 2, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Ruvuma
baada ya kuwasili kwenye uwanja ndege wa Songea kuanza ziara ya
kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma.
Waziri Mkuu amesema
Halmashuri zote za mkoa huo zijikite katika kujenga madarasa ili wanafunzi wote
waliofaulu ambao wanatakiwa kwenda sekondari waende.
Amesema Serikali ya awamu ya
tano imedhamiria kwa dhati kuahakikisha kwamba watoto wote wenye sifa za kupata
elimu ya seondari wanapata elimu hiyo kote nchini hivyo juhudi za makusudi
lazima zifanywe na kila Halmashauri ili kutimiza azma.
Akizungumzia suala la utoro
shuleni, Waziri Mkuu amesema hilo ni moja kati ya maeneo yanayozorotesha juhudi
kubwa za Serikali za kuwapatia watoto wa Tanzania elimu
katika maeneo mengi nchini na lazima viongozi wa wilaya na mikoa wasimame
imara ili kukomesha hali hiyo.
Amesema viongozi wa ngazi
zote katika mikoa na wilaya ndiyo hasa wanaoweza kumaliza tatizo la utoro
wakishirikiana kwa karibu na wanavijiji ambao wanaishi na watoto hao na wanajua
ni watoto wangapi hawaendi shule.
Hivyo, Waziri Mkuu amewataka
viongozi hao kutoa maelekezo na miongozo itakayowabana watoto
watoro pamoja na wazazi au walezi wao kwani wanayo
mamlaka na uwezo wa kuchukuwa hatua kwa mujibu wa sheria
za nchi.
Akizungumzia zao
la korosho , Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mkoa wa Ruvuma kuwaondolea hofu
wananchi wanaolima zao hilo katika mkoa huo kwa
kuwahakikishia kwamba Serikali inazo fedha za kutosha kununua
korosho zote ziliyovunwa na wakulima.
Kuhusu ukusanyaji wa mapato
ya Serikali, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na wilaya
kubeba dhamana waliyopewa na Taifa ambayo ni pamoja na kusimamia ukusanyaji
mapato ya Serikali kwa kishirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
"Halmashauri zote na wakuu wa wilaya wasimamie kwa dhati ukusanyuaji wa
kodi."
Akiwa mkoani Ruvuma, Waziri
Mkuu kesho anatarajiwa kufungua soko la mazao la Lilambo katika wilaya ya
Songea, kufungua ghala la mazao la Mgazini na kuweka jiwe la msini
la ujenzi wa zahanati ya Luganga na kisha kuhutubia mkutano
wa hadhara.
Keshokutwa Waziri
Mkuu ataongoza kikao cha wadau wa zao la kahawa
kitakachowashirikisha pia Waziri wa Kilimo na Mrajisi wa Ushirika.
Wengine watakaoshiriki katika kikao hicho ni viongozi wa AMCOS,
UNION na viongozi wa Bodi ya kahawa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina
Mndeme wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara
ya kikazi mkoani humo, Januari 2, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakisalimiana na
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho wakati walipowasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani humo,
Januari 2, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa
Peramiho, Jenista Mhagama na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,
Christina, Mndeme.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakati
alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi
mkoani humo, Januari 2, 2018. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment