Pages

Wednesday, January 2, 2019

DKT. SALIM AHMED SALIM ALAZWA HOSPITALI, RAIS MAGUFULI NA MKEWE WAMJULIA HALI.


NA K-VIS BLOG
WAZIRI Mkuu mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim amelazwa hospitali jijini Dar es Salaam na leo Januari 2, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli, wamemtembelea kumjulia hali na kumuombea dua.
Picha za Ikulu zimemuonyesha Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth, pamoja na familia ya Dkt. Salim na wasaidizi wa Rais  wakimuombea dua pembezoni mwa kitanda alikolazwa Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi huru za Kiafrika (OAU), kwa sasa AU.
Rais Magufuli.
Picha hizo ukiwemo ukanda wa video zinamuonyesha Rais Magufuli akimsalimia Dkt, Salim na kumuuliza hali hali yake na kumpa pole. “Niliambiwa jana kuwa hali haikuwa nzuri, nikawaambia jamani mumsaidie mzee wangu apone.” Alisema kabla ya kuungana na mkewe pamoja na familia ya Dk. Salim  kumuombea dua ili apone haraka. Rais Magufuli alisema alijulishwa juu ya ugonjwa unaomsumbua na amefanyiwa upasuaji baada ya kufikishwa hospitalini hapo jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli pia anauguliwa na mama yake mzazi Bibi Suzana Magufuli anaesumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiungana na mkewe Mama Janeth Magufuli, (wapili kushoto mstari wa mbele), Mama Amne Salim Ahmed Salim, (wakwanza kushoto) ambaye ni mke wa Dkt. Salim, kumuombea dua Waziri Mkuu huyo mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kutokana na maradhi yanayomsumbua leo Januari 2, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiungana na mkewe Mama Janeth Magufuli, familia ya Dkt. Salim ikiongozwa na mkewe mama Amne Salim Ahmed Salim, kumuombea dua Waziri Mkuu huyo mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kutokana na maradhi yanayomsumbua leo Januari 2, 2019.(PICHA NA IKULU).

No comments:

Post a Comment