Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi ambao
ndio waandaaji wa Mbio za Morogoro Marathon akizungumza na wanahabari
kuhusu tukio hilo litakalo fanyika kesho katika uwanja wa Jamhuri
,kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal
Kihanga,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Morogoro ,Grace Njau na kulia ni
Fuhad Hussein ,Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ambao ndio wadhamini .
Medali zilizoandaliwa kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo ambazo zitatolewa Mbili kwa kila mshiriki .
Meneja
wa DSTV mkoa wa Morogoro ,Fuhad Hussein akizungumza juu ya zawadi za
Ving'amuzi zitakazo tolewa kwa washindi wa mbio za Km 21 na Km 5.
Mkurugenzi wa Mbio,Robert Kaliyahe akitoa ufafanuzi wa njia zitakazo tumiwa na wakimbiaji siku ya Kesho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .
WAANDAAJI wa Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathon 2018
wametangaza kutoa zawadi ya Medali mbili kwa kila mshiriki wa tukio hilo ikiwa
ni ishara ya uzinduzi rasmi wa tukio kubwa la kimichezo katika mkoa wa Morogoro.
Waandaaji hao ambao ni taasisi ya Itetet Sports Agency imetangaza zawadi hiyo jana
mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuzungumzia maandalizi ya Mbio hizo
zitakazofanyika kesho alfajiri katika uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi
alisema mbali na zawadi hizo kwa washiriki pia zipi zawadi kwa washindi wa mbio
za Kilometa 21 kwa upande wa wanaume na wanawake ambapo mshindi wa kwanza
atapata pesa taslimu kiasi cha sh 400,000 .
“Tuna mbio za Kilometa 21 pamoja na kilometa tano,lakini
uwanjani kutakuwa na mbio za kushirikisha watoto kwa maana ya mita 100 na mita
200 ,kwa kilometa 21 mbali na pesa taslimu mshindi pia atapata king’amuzi cha
DSTV kutoka kwa wadhamini kampuni ya Multchoice “alisema Mgungusi.
Alisema Mshindi wa pili atapata kiasi cha sh 250,000 pamoja
na king’amuzi cha DSTV,mshindi wa tatu akiambulia kitita cha Sh 150,000 pamoja
na king’amuzi cha DSTV huku wale watakaoshiriki mbio za Km tano mshindi wa
kwanza atapata sh 100,000 pamoja na King’amuzi cha DSTV kwa jinsia zote mbili.
“Mshindi wa pili kwa kilometa 5 tutatoa kiasi cha sh 50,000
pamoja na T shirt ,mshindi wa tatu atapata cheti pamoja na t shirt nah ii ni
kwa wanawake na wanaume watakao shiriki lakini zawadi kubwa zaidi itakuwa ni
udhamini kwa washindi watatu wa kilometa 21 na tani kwa wanaume watapata
udhamini wa kushiriki mashindano yajayo hapo mwakani”alisema Mgungusi.
Alisema katika eneo hilo washindi hao watagharamiwa ,fedha
za safari,malazi na usajili kwa ajili ya kushiriki mashindano yajayo huku
wengine washiriki wengine watakaoingia hatua ya 10 bora wao watashiriki
mashindano yajao bila kulipia ada.
Akizungumzia kuhusu maandalizi ,Mkurugenzi wa Mbio ,Robert
Kaliyahe alisema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na
upimaji wa njia zitakazotumika kwa wakimbiaji wa mbio za kilometa 21 na zile za
kilometa tano.
“ tumefanya maandalizi ya kutosha katika mbio hizi,tayari
tumewasiliana na wenzetu wa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kwa
ajili ya kuhakikisha usalama kwa wakimbiaji wakati wa kuanza mbio pale uwanja wa Jamhuri na baada ya mbio kuhitimishwa.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro ,Pascal Kihanga
amesema mkoa wa Morogoro unakwenda kuandika historia nyingine kwa kuuingiza
mkoa huo katika medani ya mchezo wa riadha kwa kuanzisha mashindano ya Morogoro
Marathoni.
“Mrogoro inavivutio vingi ambavyo vimekuwa havitangazwi
lakini kwa kupitia mashindano haya tutapata fursa mpya ya kutangaza vivutio
vyetu ambavyo vitaendelea kuutangaza vyema mkoa wetu wa Morogoro.”alisema
Kihanga .
Mbio za Morogoro Marathon 2018 zinafanyika kwa mara ya
kwanza katika mkoa wa Morogoro huku watu zaidi ya 3000 wakitazamiwa kuanza
kukimbia kuanzia majira ya saa 12:30 na kwamba zoezi la usajili kwa wakimbiaji
linaendelea katika vituo mbalimbali nchini na litafungwa saa 12:00 siku ya
tukio..
No comments:
Post a Comment