Pages

Sunday, December 2, 2018

WAZIRI MKUU AZINDUA MKAKATI WA KUDHIBITI UKIMWI


 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Seleman Jaffo nakala ya Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 leo tarehe 01 Desmba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama,  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Mussa Sima na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo. Mkakati huo unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01 Desemba 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alipowasili katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01 Desemba 2018. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustine Kamuzora.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya mabanda yaliyokuwa yakionyesha shughuli mbalmbali zinazoendeshwa na wadau alipotembelea mabanda hayo wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01 Desemba 2018 jijini Dodoma.



Baadhi ya waandamanaji toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora wakipita katiika maandamano wakati wa hafla ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01 Desemba 2018 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01, Desemba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01, Desemba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01, Desemba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.

 Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaosihi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), Bi. Leticia Mourice akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani leo tarehe 01, Desemba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 leo tarehe 01 Desmba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama,  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Mussa Sima. Mkakati huo unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez nakala ya Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 leo tarehe 01 Desmba 2018 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Muwakilishi  Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI   Duniani (UNAIDS) Dkt. Leo  Zekeng, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile. Mkakati huo unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa masuala ya Ukimwi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo. (Picha na Frank Shija - MAELEZO)NA OWM, DODOMA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezinduaMkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2018/19 - 2022/23 ambao unatarajia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 85 ifikapo mwaka 2023.Matokeo mengine yanayotarajiwa kufikiwa kutokana na mkakati huo ni kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto kwa chini ya asilimia 5 ifikapo mwaka 2023 na chini ya asilimia 2 ifikapo mwaka 2030.Waziri Mkuu amezindua mkakati huo leo (Jumamosi, Desemba 1, 2018) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma na kusema kuwa matayarisho yake yamezingatia matokeo ya mapitio ya Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI 2013/14 – 2017/18.Amesema mbali na matokeo hayo pia mkakati huo utawezesha kupungua kwa vifo vinavyohusiana na ukimwi  kwa asilimia  50 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 70 ifikapo mwaka  2023 na kupunguza unyanyapaa na ubaguzi ifikapo 2023 na kuelekea kutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo Waziri Mkuu amesema mkakati huo umewianisha na kupanga programu mbalimbali zinazosaidia mwitikio wa Taifa zikiwemo afua zinazotekelezwa kupitia mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa uKIMWI (PEPFAR).“Pia Mfuko wa Dunia wa kudhibiti UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Globa Fund) na jitihada nyingine za makubaliano ya ushirikiano baina ya nchi mbalimbali na ili kupata matokeo mazuri tunapaswa kuimarisha mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kufuata na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.” Kadhalika, Waziri Mkuu amesema maadhimisho hayo husaidia kubaini changamoto, mafanikio na hivyo, kuja na mikakati ya kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI. “Siku hii hutoa fursa kote Duniani kutafakari kwa mara nyingine kuhusu tulipotoka, tulipo na tunapokwenda katika mapambano ya UKIMWI kwenye jamii zetu.”Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu faida za kampeni ya FURAHA YANGU aliyoizindua mwezi Juni mwaka huu, ambapo aliagiza mikoa yote kufanya uzinduzi wa kampeni hiyo kwenye ngazi za mikoa na hata wilaya. Amsematakwimu zinaonesha kuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya FURAHA YANGU katika mikoa yote nchini jumla ya wananchi 262,114 walijitokeza kupima VVU, wakiwemo wanawake 136,389 na wanaume 125,725.Natoa wito kwa Mikoa na Wilaya zote kuwa kampeni hii iwe endelevu. Viongozi katika ngazi mbalimbali tuungane kwenye uhamasishaji wa jambo hili kwani vita dhidi ya VVU na UKIMWI inahitaji dhamira ya dhati na tafakuri ya kina katika kujilinda dhidi ya maambukizi mapya.”Waziri Mkuu amewahakikishia kuwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kutekeleza na kuboresha huduma za upimaji wa Virusi Vya UKIMWI, kuzuia maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, matibabu ya magonjwa nyemelezi na kupiga vita unyanyapaa wa aina zote kwa WAVIU.

No comments:

Post a Comment