Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa, (katikati, walio
kaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)
pamoja na watumishi wa Shirika hilo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo katika
Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Sam Kamanga,
akipongeza
juhudi za Serikali katika kuhakikisha Shirika hilo linaimarika, wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bodi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw . Laston Thomas Msongole,
akiwaeleza watumishi wa Shirika hilo kuhusu kuendelea kufanyakazi kwa ufanisi,
wakati utaratibu wa kuiondoa NIC katika orodha ya Mashirika yanayotakiwa
kubinafsishwa ukiendelea.
Baadhi
ya watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika
la Bima la Taifa (NIC) Bw . Laston Thomas Msongole (kulia) wakimsikiliza kwa
makini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa,
alipokuwa akielezea hatua za Serikali katika kuiondoa NIC, katika
orodha ya Mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika
Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Na WFM. Dodoma
Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kuliimarisha Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuliondoa katika
utaratibu wa ubinafsishaji ambao uliwekwa awali.
Hayo yamebainishwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bi Susana Mkapa, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor
Mpango, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tisa wa baraza la Wafanyakazi wa
Shirika la Bima la Taifa Jijini Dodoma.
Bi Susana alisema kuwa,
hatua za kuliondoa Shirika la NIC katika utaratibu wa ubinafsishaji zimefikia
hatua nzuri ambapo utahitimishwa kwa kuandaa hati ya kisheria.
“Wizara ya Fedha na
Mipango imeongeza muda wa mikataba ya kazi kwa watumishi kwa miezi mitatu,
hivyo mawasiliano rasmi kuhusu mikataba hiyo yatafanyika, nawaomba watumishi
muendelee kufanya kazi na kuwajibika wakati taratibu hizi za kuliondoa Shirika
katika ubinafsishaji zikikamilika”. Alieleza Bi. Mkapa.
Vilevile alisema kuwa,
maamuzi ya Mashirika na Taasisi za Serikali kupata huduma za Bima kupitia
Shirika la Bima la Taifa ni ya Kisera na yanahusisha mamlaka mbalimbali, hivyo
amelitaka Shirika hilo liendelee kufanya kazi kwa ushindani, kuongeza ufanisi,
ubunifu na kuondokana na fikra za kufanyakazi kwa mazoea.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga alisema kuwa baadhi ya Taasisi na Mashirika ya
Umma yanasita kutumia Bima za Shirika hilo kwa kuwa hakuna tamko rasmi ambalo
linasimamia utekelezaji hivyo kuiomba Serikali
kutoa tamko hilo.
Pia ameiomba Serikali
kuliongezea Shirika hilo mtaji kwa kuwa uliopo wa kiasi cha Sh. bilioni 2.9, ni
mdogo na haukidhi katika kuimarisha Shirika hilo kwa utoaji wa bidhaa
mbalimbali kulingana na uhitaji wa Soko.
Naibu Katibu Mkuu Bi Susan
Mkapa alilipongeza Shirika la NIC kwa kuwa na Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ambao
utekelezaji wa matakwa ya sheria na kanuni zinazosimamia mahusiano kazini kati
ya Menejimenti na wafanyakazi, na ushirikishwaji katika uendeshaji wa Taasisi,
hivyo akawataka watumishi hao kuhakikisha wanatoa ushauri utakao imarisha
taasisi hiyo na kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment