Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akizungumza
na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji (TBC)Dkt. Ayoub Rioba wakati Mkurugenzi
huyo alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Jijini Dodoma, wa
kwanza ni Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kati TBC , Ndugu Bakari Msulwa
Katibu wa Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai
akiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji (TBC) Dkt. Ayoub Rioba wakati
Mkurugenzi huyo alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Jijini
Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akielezea jambo mbele ya Kamati hiyo
ilipokuwa ikijadili Taarifa za Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa
mwaka 2019/2020 na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa
Fedha 2019/20 – 2021/22 katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Ukumbi wa
Msekwa Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakijadili
Taarifa za Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020 na
Mwongozo wa maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2019/20 – 2021/22
kataika Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment