Na Francis Godwin,Iringa
TAASISI ya kuzuia na kupambana
na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani mstakihi meya
wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Alex Kimbe kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) makosa mawili ya jinai kuomba
na kupokea rushwa .
Kaimu kamanda wa takukuru
mkoa wa Iringa Mweli Kilimali akizungumza leo na vyombo vya
habari ofisibni kwake alisema kuwa meya huyo alipokea kiasi cha
shilingi milioni 2 kutoka kwa mteja wao .
Alisema kuwa tukio la kukamatwa
meya huyo lilitokea Novemba 15 mwaka huu majira ya
saa 12 jioni
katika Hotel ya Gentle Hills mjini Iringa .
Kuwa meya huyo ambae ni diwani
wa kata ya Isakalilo aliokea pesa hizo kinyume na kifungu cha
15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.
Alisema meya Kimbe alipokea
fedha hizo za mtego wa rushwa akiwa kwenye gari yake aina ya
nadia yenye rangi ya Marron ikiwa na namba za usajili T 456 CKD
iliyokuwa imeegeshwa katika eneo la kuegesha magari kwenye hoteli
hiyo .
“ Maafisa wa takukuru waliweza
kumfuatilia meya huyo kwa muda mrefu na hivyo kuweza kumkamata
akiwa amekwisha pokea fedha hizo za mtego kutoka kwa mtoa taarifa
wao “
Kilimali alisema kuwa awali
walipokea taarifa ya kuwepo kwa ushawishi wa kutoka kwa meya huyo
kwenda kwa mmoja kati ya wakandarasi wanaoendesha tenda katika
Manispaa ya Iringa ili muda ukiisha apate nafasi ya kupata tenda
husika .
Hivyo meya huyo alimuomba mtoa
taarifa rushwa na shilingi milioni 10 na baada ya mtoa taarifa
kujitetea hatokuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo mtuhumiwa alikubali
kupokea shilingi milioni 2.
Akiwa mahakamani Mwendesha
mashtaka upande wa jamhuri Restuta Samson alisema hamakamani
hapo jana kuwa Kimbe anashitakiwa makosa hayo mawili likiwemo
la kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Nance Nyalusi
kama zawadi baada ya kupata zabuni ya kukusanya ushuru stendi kuu ya
mabasi mjini Iringa .
Kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo kinyume na sheria kwa meya kuomba zawadi hiyo kutoka kwa mzabuni huyo .
Wakati shitaka la pili ni
mshitakiwa amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kupokea rushwa
kutoka kwa Nance Nyalusi .
Hata hivyo mshitakiwa huyo
aliweza kukana makosa yote yanayomkabili kuwa si ya kweli na kwa
kuwa upande wa wakili wa jamhuri katika kesi hiyo uliieleza
mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika na hauna
pingamizi juu ya dhamana ya mshitakiwa .
Hakimu wa mahakama hiyo Liad Chamshana
alisema hamaka yake inamtaka mshitakiwa kusaini dhamana ya
maadishi ya shilingi milioni 10 pamoja na kuwa na wadhamini wawili
mashariti ambayo yalitekelezwa na mshitakiwa kuachiwa kwa dhamana
.
Akizungumza nje ya mahakama na
waandishi wa habari wakili anayemtetea Kimbe Lutebuka Samson Antony
alisema kuwa kosa la kwanza linalomkabili mtaja wake ni kudhaniwa
kuomba rushwa huku kosa la pili ni la kudhaniwa kupokea rushwa
kesi hiyo itatajwa tena Desemba 5 mwaka huu .
No comments:
Post a Comment