Waziri wa Maji, Profesa. Makame
Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu
ufunguzi wa mkutano wa 21 wa baraza la mawaziri wa maji katika nchi
bonde la mto Nile zilizopo ukanda wa maziwa makuu utakaofanyika jijini
Dar es salaam Novemba 22 mwaka huu.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia
mkutano baina yao na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (hayupo
pichani) leo jijini Dodoma kuhusu ufunguzi wa mkutano wa 21 wa baraza la
mawaziri wa maji katika nchi bonde la mto Nile zilizopo ukanda wa
maziwa makuu utakaofanyika jijini Dar es salaam Novemba 22 mwaka huu.
Na Mpiga Picha ALEX SONNA
………………….
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma
Rais John Magufuli anatarajia
kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa baraza la mawaziri
wa maji katika nchi wanachama bonde la mto Nile zilizopo kwenye ukanda
wa maziwa makuu unaotarajia kufanyika jijini Dar es salaam Novemba 22
mwaka huu.
Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na kupitia utekelezaji wa masula mbalimbali ya
miradi,kupokea taarifa ya
utendaji,hali ya ulipaji wa michango ya kila mwaka kwa kila nchi
mwanachama na tathimini ya watumishi wa sekretariati ya NELSAP.Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na kupitia utekelezaji wa masula mbalimbali ya
Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Waziri wa maji Prof. Makame Mbarawa alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa maji wa nchi za bonde la mto Nile za ukanda wa maziwa makuu ukiwa ni mkutano wa kawaida wa kiutendaji.
Prof.Mbarawa amesema kuwa baraza la mawaziri wa maji ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi katika kusimamia na kuendesha shughuli za bonde la mto Nile katika ukanda wa maziwa makuu na mkutano huu unaofanyika mara moja kwa kila mwaka hufuata mzunguko katika nchi wanachama.
Hata hivyo Prof.Mbarawa amesema kuwa mkutano huo wa baraza la mawaziri wa maji utatanguliwa na vikao vya wataalamu vitakavyoanza Novemba 20 hadi 21 jijini Dar es salaam.
“Vikao hivyo vya wataalam ambavyo ni vya kiutendaji hufanyika mara mbili kwa mwaka kufuata mzunguko katika nchi wanachama”amesema Prof Mbarawa.
Aidha amesisitiza kuwa ushirikiano wa nchi za bonde la mto Nile ni wa muda mrefu ambao ulianza tangu mwaka 1960 na ilipofika Februari 22 1999 nchi wanachama ziliunda Taasisi ya mpito iitwayo Nile Basin Initiative-NBI.
Hata hivyo ameongeza kuwa
malengo ya ushirikiano huu ni kufikia uanzishwaji wa kamisheni ya Bonde
la mto Nile ambayo mchakato wake unaendelea.
Prof.Mbarawa ameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 11 za Bonde la mto Nile zinazoshirikiana katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za Bonde la mto huo chini ya mwamvuli wa Nile Basin Initiative (NBI).
Aidha alizitaja nchi nyingine kuwa ni Burundi,Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo,Misri,Ethiopia,Kenya,Rwanda,Sudani ya kusini,Sudani,Uganda na Eritrea ambayo ni mtazamaji.
Amesema kuwa ushirikiano huo unafaida kubwa ambapo nchi wanachama zinafaidika na maji ya mto Nile kwa kuwa na haki sawa ya matumizi.
Prof.Mbarawa amesema kuwa katika mkutano huo Tanzania ambayo ndiyo mwenyekiti kwa sasa itakabidhi kijiti hicho kwa nchi ya Uganda.

No comments:
Post a Comment