MSANII wa
filamu Wema Sepetu, maarufu kama “Madame” amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja
(1) jela baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa ya kulevya aina ya
Bangi.
Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imetoa hukumu hiyo leo Julai 20, 2018
na kwamba Wema pia anayo nafasi ya kulipa faini ya shilingi milioni 2 ili
kukwepa kifungo hicho.
Aidha
Mahakama imewaachia huru watumishi wake wawili baada ya kuwaona hawana hatia.
Msanii Wema
Sepetu alijikuta matatani baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul
Makonda, kuanzisha operesheni kali ya kuwasaka watumiaji, wauzaji, waingizaji
na wasambazaji wa dawa za kulevya za aina zote, ambapo watu kadhaa walijikuta
matatani akiwemo Wema.
Hata hivyo Wema aliweza kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Hata hivyo Wema aliweza kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.

No comments:
Post a Comment