WAZIRI wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu,
ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (MAWENI), na kujionea
changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo kongwe kabisa hapa nchini.
Mhe. Ummy
Mwalimu ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa “Ameridhishwa na hali ya
utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni. Ingawa kuna
changamoto ya Uhaba wa watumishi na uchakavu wa miundombinu.” Anasema Mhe. Ummy
mwalimu.
Mhe. Waziri
amesema, Mwaka huu 2018/19 Serikali imetenga shs bilioni 1.1 kwa ajili ya
kuboresha Miundombinu. Pia mwezi huuwa saba (July) Wizara yake itapeleka
watumishi wapya 34 wakiwemo madaktari 7 na wauguzi 17.
Aidha Mhe. Waziri ameonyesha
kuchukizwa na kitendo cha uongozi wa Hospitali hiyo wa kuwatoza fedha watoto
chini ya miaka mitano kitu ambacho ni kinyume na miongozio ya wizara hoyo.
“Naagzia ni
marufuku kuwatoza fedha wagonjwa wenye umri chini ya miaka mitano za vipimo au
kumuona daktari.” Alisema na kuamuru mkazi mmoja aliyefika hospitalini hapo
akiwa na motto wake mwenye umri chini ya miaka mitano (5), ambaye alilipa fedha
za kumuona daktari na vipimo, arudishiwe fedha zake mara moja.
Hata hivyo
Mheshimiwa Waziri amefurahi kuona Madaktari Bingwa wakitoa huduma ktk Hospitali
hiyo.
Aidha Mhe. Waziri amesema Wizara yake imedhamiria kuboresha
huduma ktk Hospitali za Rufaa za Mikoa. "Moja ya mikakati yetu ni kuhakikisha
uwepo wa Madaktari Bingwa ktk fani za kipaumbele ambazo ni Upasuaji (General
Surgery), Magonjwa ya Wanawake na Uzazi (Obstetrics & Gynaecology),
Magonjwa ya Watoto (Paediatrics & Child Health), Magonjwa ya ndani
(Internal Medicine), Magonjwa ya Kinywa na Meno (Dentistry) na Radiolojia
(Radiology). Hivi sasa tunaweka mazingira mazuri kuvutia Madaktari Bingwa na
Watumishi wengine wa Afya kufanya kazi mikoa ya pembezoni ikiwemo Kigoma. Aidha
Ninawataka Watumishi wapya wote waliopangwa kufanya kazi mikoa ya pembezoni
ikiwemo Kigoma waripoti katika Vituo Vyao. Hatutabadilisha Vituo. Utumishi wa
Umma ni Popote. Muhimu zaidi watu wa mikoa hii nao wana haki ya kupata huduma
bora za Afya" Alibainisha
Mhe.
Waziri Umy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Osmund
Dyegura (Upasuaji), Dkt. Lameck Mdengo (Magonjwa ya Wanawake na Uzazi), Dlt.
Macrive Yakayashi (Magonjwa ya Watoto), Dlt. Sunday
Dominico (Magonjwa ya Wanawake na Uzazi
Waziri wa Afya,Maendekeo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipanda kivuko kuelekea kijiji cha Mwamgongo ziwa Tanganyika kuweka jiwe la Msingi katika Zahanati ya kijiji hicho pia kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika zahanati hiyo.Waziri Ummy Mwalimu akiendelea na ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Kigoma
Waziri wa Afya,Maendekeo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipanda kivuko kuelekea kijiji cha Mwamgongo ziwa Tanganyika kuweka jiwe la Msingi katika Zahanati ya kijiji hicho pia kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika zahanati hiyo.Waziri Ummy Mwalimu akiendelea na ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Kigoma





No comments:
Post a Comment