Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akikabidhi
Televisheni kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile kwa ajili ya klabu ya watoto katika
kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
***
ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA
Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akiteta jambo na Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile
wakati wakielekea katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya kushuhudia kazi zinazofanywa na
AGPAHI katika kuimarisha huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na
VVU.Kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa
Mara, Alio Hussein.- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akielekea katika
kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Mara,Dkt. Joachim Eyembe akitoa taarifa kuhusu huduma
za afya katika hospitali hiyo kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara na kuupongeza uongozi wa hospitali
hiyo kwa kuimarisha huduma za afya na kupunguza malalamiko kutoka kwa
wagonjwa.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt.
Sekela Mwakyusa akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na AGPAHI katika
kuimarisha huduma za tiba za matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi Vya
UKIMWI mkoani Mara. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus
Manyinyi Mathayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akifafanua kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na AGPAHI mkoani Mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt.
Sekela Mwakyusa akiwasisitiza viongozi wa serikali kuendelea
kushirikiana na AGPAHI katika kudhibiti maambukizi ya VVU.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt.
Sekela Mwakyusa akiishukuru serikali kwa kuwapa fursa ya kuwatumikia
Watanzania kuleta mabadiliko chanya kwenye masuala ya afya hasa UKIMWI.
Vifaa vilivyotolewa na AGPAHI kwa ajili
ya klabu ya watoto na vijana wa kituo cha tiba na matunzo katika
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.Vifaa hivyo ni
televisheni,mipira,mikeka,viti na vitabu.
Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine
Ndugulile,Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Manyinyi
Mathayo,Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara,Dkt.
Joachim Eyembe na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Anney
wakiangalia vifaa vilivyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya klabu ya watoto
na vijana katika kituo cha tiba na matunzo cha hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Mara.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akielezea kuhusu vifaa hivyo ambavyo ni
pamoja na vifaa vya michezo.Alisema mbali na kutoa vifaa vya michezo pia
wameboresha viwanja vya michezo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Mara.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI,
Dkt. Sekela Mwakyusa akikabidhi Televisheni kwa Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile
kwa ajili ya klabu ya watoto katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI,
Dkt. Sekela Mwakyusa akikabidhi Televisheni kwa Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile
kwa ajili ya klabu ya watoto katika kituo cha tiba na matunzo (CTC) cha
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kushoto ni Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile
akikabidhi televisheni kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Mara,Dkt. Joachim Eyembe kwa ajili ya klabu ya watoto katika kituo
cha tiba na matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi vitabu
kwa mmoja wa vijana kutoka klabu ya vijana katika CTC ya hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Mara.
Kijana akiishukuru AGPAHI kwa kuwapatia vifaa vya michezo.
Vijana kutoka CTC ya hospitali ya Rufaa
ya mkoa wa Mara wakionesha igizo linalotoa elimu kuhusu umuhimu wa kuwa
wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza makali ya VVU.
Wafanyakazi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara wakifuatilia igizo.
Mshauri wa Watu Wanaoishi na VVU Nehemia
Kaswala Mtumi anayeishi na maambukizi ya VVU tangu mwaka 1995 na mke
mmoja na watoto watano wote hawana maambukizi ya VVU akielezea namna
wanavyoshirikiana na AGPAHI na serikali katika kuhamasisha masuala ya
afya kwa watu wanaoishi na VVU,uzazi wa mpango,TB na uchunguzi wa
saratani ya shingo ya mlango wa kizazi,upimaji wa VVU nyumba kwa nyumba
na uundaji wa vikundi vya WAVIU.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiandika dondoo
muhimu wakati Mshauri wa Watu Wanaoishi na VVU Nehemia Kaswala Mtumi
akitoa salamu za WAVIU Washauri kutoka hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Mara.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Anney akimweleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt.
Sekela Mwakyusa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakifurahia jambo.
Mshauri wa Watu Wanaoishi na VVU Nehemia
Kaswala Mtumi akikabidhi taarifa yake kwa Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Kijana akisoma risala kuhusu klabu ya
watoto kutoka Kituo cha tiba na Matunzo (CTC) cha hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Mara.Alisema tangu AGPAHI ianze kufadhili klabu hiyo mwaka 2017
wamefanikiwa kuongeza uelewa kuhusu VVU,UKIMWI, lishe bora,umuhimu wa
mazoezi na ufuasi mzuri wa dawa. Aidha aliitaka serikali na wadau
kuielimisha jamii kuacha unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU kwani
wanahitaji upendo badala ya unyanyapaa.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza kwenye
kituo cha tiba na matunzo (CTC) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Mara. Aliwataka watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuwa wafuasi wazuri
wa dawa na wale ambao ambao hajapima afya hususani wanaume kujitokeza
kupima ili wajue hali ya afya zao.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile pia aliitaka jamii
kuacha tabia ya kunyanyapaa watu waliopata maambukizi ya VVU na
kusisitiza kuwa dawa za kufubaza makali ya VVU zipo za kutosha.
Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara
Dkt. Francis Mwanisi akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Vijana kutoka CTC ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara wakicheza mchezo wa kuchangamsha akili na mwili 'Chicken Dance'.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akicheza na watoto
mchezo wa kuchangamsha akili na mwili 'Chicken Dance'.
Mchezo wa kuchangamsha akili na mwili 'Chicken Dance' ukiendelea.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile ameipongeza asasi
ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare
Initiative (AGPAHI) kwa kuimarisha huduma za tiba na matunzo kwa
watu wanaoishi na VVU mkoani Mara.
watu wanaoishi na VVU mkoani Mara.
Dkt. Ndugulile alitoa pongezi hizo Julai
19,2018 wakati akiwa katika katika ziara ya kikazi mkoani Mara na
kushuhudia kazi zinazofanywa na AGPAHI katika hospitali ya RufAudienceaa ya mkoa
wa Mara katika kuhudumia watu wanaoishi na VVU ambapo pia alipokea
vifaa vya michezo vilivyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya klabu ya watoto
iliyopo katika hospitali hiyo.
"Nimekuja kupata ushuhuda wa kazi kubwa
ambayo wadau wetu wa maendeleo AGPAHI katika kudhibiti maambukizi ya
Ukimwi,niwashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya kwa
kushirikiana na serikali katika kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI, na
tunawashukuru kwa misaada mbalimbali mnayotupatia”,alisema Dkt.
Ndugulile.
"Serikali inafarijika sana kuona wadau
wanakuwa na mchango mkubwa katika kudhibiti UKIMWI, kama wadau wa
maendeleo tunatarajia wataziba mapengo pale serikali haijafika
kinachotakiwa ni kushirikiana, tunataka NGO's zote zinazofanya kazi
katika mkoa wa Mara ziendane na vipaumbele vya mkoa”,aliongeza.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema serikali
imedhamiria kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 asilimia 90% ya watu
wenye maambukizi ya VVU wanafikiwa na kupimwa,ambapo asilimia 90% ya
walioathirika wanapewa dawa za kufubaza virusi na asilimia 90% ya
watakaotumia dawa hizo hawataweza kuwaambukiza watu wengine kwa sababu
virusi vitakuwa vimefubazwa na tiba hiyo.
“Mpaka sasa tumewafikia Watanzania
takribani milioni 1.4 wanaohisiwa kuwa wanaishi na VVU, bado tunapambana
kuwafikia laki nne ambao hatujawafikia, lakini sambamba na hayo
tunaendelea kupambana kuhakikisha maambukizi mapya tunayadhibiti kwa
kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kudhibiti maambukizi kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto”,alisema.
Alisema serikali itaendelea kuhakikisha
kuwa dawa za kufubaza makali ya VVU zinaendelea kupatikana kwa asilimia
100 huku akiwasisitiza wanaume kujitokeza kupima afya zao ili kubaini
kama wana maambukizi ya VVU na wakibainika wameambukizwa basi waanze
kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU.
Akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na
AGPAHI, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa alisema
katika mkoa wa Mara,wanatoa huduma katika vituo 113 vya kutolea huduma
za afya,68 vya huduma ya matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na VVU
(CTC) na vingine 45 vya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto (PMTCT).
“Tunatekeleza mradi wa Boresha kwa
ufadhili wa serikali ya Marekani kupitia shirika la Centres for Disease
Control (CDC),ambapo mradi huu unatoa huduma za kinga,tiba na matunzo
kwa watu wanaoishi na VVU”,alisema.
Dkt. Sekela alibainisha kuwa kuanzia
mwezi Oktoba 2017 hadi Machi 2018,AGPAHI imefanikiwa kupima watu 162,389
ambapo kati yao 4,482 sawa na asilimia 2.7 waligundulika kuwa na
maambukizi ya VVU wakiwemo watoto 265.
“Katika kipindi hicho pia watoto 988
walizaliwa na akina mama wenye VVU lakini kutokana na huduma za kukinga
watoto dhidi ya maambukizi kutoka kwa mama, watoto 934 sawa na 98%
hawakuwa na maambukizi, na 16 waliopata maambukizi wanaendelea kupata
huduma za VVU”,alieleza Dkt. Sekela.
“AGPAHI ilipoanza kutekeleza mradi wa
Boresha hapa Mara Oktoba 2016 kulikuwa na watu 25,821 wanaopata huduma
za VVU na UKIMWI,lakini kwa kushirikiana na serikali tumeweza kuwafikia
watu 31,729 ‘wanaume 9,202 (29%),wanawake 22,527 na watoto
1,664,tunaendelea na upimaji hasa tukilenga kuwatambua wanaume wenye
maambukizi ili waanze kupata huduma hizi muhimu”,alifafanua Dkt.
Sekela.
Aidha aliongeza kuwa katika kuunga mkono
juhudi za serikali za kupambana na upungufu wa wafanya kazi kwa kada ya
afya,AGPAHI imewezesha ajira kwa watumishi wapatao 201 kati yao 118 ni
makarani takwimu na 83 ni maafisa tabibu,wataalam wa maabara na
wauguzi.
Dkt. Sekela alisema mbali na kuwajengea
uwezo Washauri wa Watu Wanaoishi na VVU 123 na kuanzisha vikundi vya
WAVIU pia AGPAHI inaendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vifaa vya
michezo,televisheni na kutengeneza vifaa vya michezo.
“Kupitia mradi wa Boresha AGPAHI imetoa
kompyuta 86 kwa ajili ya kurahisisha mfumo wa takwimu katika halmashauri
zote za mkoa wa Mara,tumetoa Cryotherapy mashines kwa ajili ya matibabu
ya dalili za mwanzo za saratani ya mlango wa kizazi,solar panels kwenye
vituo vya afya,kuboresha vituo vya afya,majokofu ya kutunzia
dawa,darubini na vitu mbalimbali”,aliongeza.
Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare
Initiative (AGPAHI) ni asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali iliyoanza
kushirikiana na serikali ya Tanzania katika juhudi za kutokomeza VVU na
UKIMWI kwa watoto tangu 2011 katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu kisha
Mwanza,Geita,Mara na Tanga kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia
vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment