Picha
ya pamoja ya Waheshimiwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma na Wafanyakazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum juu ya mradi wa
pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa na Wabunge hao ulioandaliwa na UN na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mbunge
wa Kigoma Mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Mh. Zitto Kabwe akifafanua
jambo wakati wa majadiliano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa
Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mkuu
wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga (kulia) akifungua
mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma juu ya mradi wa pamoja na
Umoja wa Mataifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa
Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo.
Mbunge
wa Kasulu Vijijini –CCM , Mh. Augustine Vuma akichangia maoni mara baada ya
kupitishwa kwenye maeneo ya mradi wa pamoja wa Kigoma wa Umoja wa Mataifa wakati
wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati), Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa
Kigoma, Evance Siangicha (kushoto) pamoja na Mchambuzi Mratibu wa Umoja wa
Mataifa (UN Coordination Analyst )nchini, Kanali Rankho wakipitia Programu ya
Pamoja ya Kigoma na Umoja wa Mataifa kabla ya kuanza kwa mkutano uliohusisha
Wabunge wa mkoa wa Kigoma na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho kutoka Umoja wa
Mataifa wakati wa mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma juu ya
mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa (UN-KJP) uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo na kushoto ni Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani wa waheshimiwa wabunge
wa mkoa wa Kigoma kwa kushiriki mkutano maalum juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma
na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano huo na Wabunge hao ulioandaliwa na UN na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kusini-CCM, Mh. Hasna Mwilima akichangia maoni yake katika
eneo la muundo wa usimamizi katika Programu ya pamoja ya Kigoma na Umoja wa
Mataifa mara baada ya kupokea muhtasari wakati wa wa mkutano maalum na Wabunge
wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
za Umoja wa Mataifa.
Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia uwekezaji
katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF),
Imanuel Muro akifafanua jambo kwenye maeneo ambayo UNCDF yanahusika wakati wa
majadiliano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa
mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mbunge
wa jimbo la Buhingwe, Mh. Albert Obama akichangia maoni wakati wa majadiliano
juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum
na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha (kulia) akiwasilisha muhtasari wa
mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma wakati wa
mkutano maalum ulioandaliwa juu ya mradi huo wa pamoja uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Faith Shayo (kulia) akielezea kuhusu mradi wa
UNESCO kwa kushirikiana na UN Women pamoja na UNFPA unaofadhiliwa na Shirika la
Misaada la Korea (KOICA) katika eneo la elimu wakati wa mkutano juu ya mradi wa
pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa
mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Umoja wa Mataifa.
Pichani
ni Waheshimiwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma na Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa walioshiriki mkutano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa
Mataifa ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Umoja wa Mataifa.
NA
MWANDISHI WETU
WABUNGE
wa mkoa wa Kigoma walipata nafasi ya kutaarifiwa mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma
na Umoja wa Mataifa ambao umejikita katika kutekeleza Mpango wa Taifa wa
Maendeleo na pia kutekeleza shughuli mbali mbali zinazolenga kufikia malengo
endelevu ya dunia.
Akifungua
mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga
aliwataka washiriki wa mkutano huo kufuatilia kwa makini hatua iliyofikiwa ya
mradi huo na kutoa mapendekezo yao.
Baadhi
ya shughuli za mradi huo zimeanza kutekelezwa hususan katika maeneo ya Kilimo,
uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi, kutokomeza vitendo vya unyanyasaji
wa kijinsia kwa watoto na kina mama pamoja na elimu.
Mkuu
huyo wa mkoa aliwataka waheshimiwa wabunge kutumia fursa waliyoipata kupokea
taarifa kuhusu mradi na kutoa ushauri wa namna ya kufanikisha malengo
yaliyowekwa ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma.
“Mkoa
wa Kigoma ni Mkubwa na tunatamani kuona mradi huu unapanuka kujumuisha wilaya
zote na pia sekta nyingine muhimu kama afya. “ alisema Maganga ambaye alisema
kama serikali wako tayari kushirikiana na wadau wote wenye mapenzi na mkoa wa
Kigoma wataliona hilo.
Katika
mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez na wadau wengine wa maendeleo, misingi imara ya
ushirikiano kwa ufanikishaji wa maendeleo ya mkoa wa Kigoma kwa ujumla
yalizungumzwa na kuafikiwa.
Mkuu
huyo wa mkoa pia alimshukuru Bw. Alvaro, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Tanzania na waandaji wa kikao hicho.
Kwa
mujibu wa mkuu huyo wa mkoa lengo kuu la kikao ni kujadiliana juu ya Mpango wa
Pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Mkoa wa Kigoma na pia kujadili masuala
mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mkoa huo.
Kikao
hicho cha wabunge kiliombwa kwenye Mkutano wa RCC wa mwaka jana na kutokana na
kutokupatikana fursa kiliahirishwa mara kwa mara .
Mashirika
16 ya Umoja wa Mataifa Tanzania yanashirikiana na wadau wengine wa maendeleo na
serikali kutekeleza mradi wa pamoja ambao utashughulikia masuala ya wenyeji na
wakimbizi kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
“Shukrani
za kipekee zimwendee Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti
mwenza wa kamati ya uongozi ya mradi huu, Bw. Alvaro kwa mapenzi aliyo nayo kwa
mkoa wa Kigoma hadi kuwa chachu ya uanzishwaji wa mradi huu. “ alisema Maganga
Naye
Mratibu huyo Alvaro Rodriguez alisema
kwamba Umoja wa Mataifa wataendelea kuisaidia Tanzania kwa kutambua umuhimu uliopo.
“Tanzania,
na hasa Mkoa wa Kigoma, imepokea maelfu ya wakimbizi kutoka nchi jirani kwa
miongo mingi. Kitendo hiki cha ukarimu wa kuwapokea watu wanaoteseka, na
kukimbia migogoro kinafanywa kwa niaba ya jumuiya ya kimataifa, nasi
tunawapongeza sana kwa moyo huo,” alisema
na kuongeza kuwa changamoto kwa jamii ya wenyeji, kunalazimisha uwepo
umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kujinusuru.
Kujinusuru,
ndio chombo kikuu cha kinga kwa mkimbizi, na ni kigezo muhimu katika hatua za
kiutu, ili kutoa mwitikio kwa mgogoro unaofukuta wa mahitaji ya kiutu.
Alisema
kwamba UN wamegundua kwamba hakuna njia ya kuwahakikishia wakimbizi kinga kama
mahitaji, maslahi na matamanio yao yataifanya jamii ya wenyeji kuchoka na
kuibua mivutano kati ya jamii tofauti.
Alisema
kuanzishwa kwa Mpango wa Pamoja wa Kigoma ni jitihada muhimu inayolenga
kuunganisha mpango wa misaada ya kibinaadam, na ule wa kuleta maendeleo na
kupunguza mzigo unaozielemea jamii za wenyeji.
Programu
hiyo kwa sasa inaweka mkazo katika maeneo sita, yaani, nishati na mazingira
endelevu; uwezeshaji kiuchumi vijana na wanawake; ukatili dhidi ya wanawake na
watoto; elimu; maji, usafi na usafi binafsi (WASH); na, kilimo. Utekelezaji wa
shughuli zilizo chini ya maeneo haya, unaendana na mipango ya sasa ya kitaifa
na ngazi ya mkoa.
No comments:
Post a Comment