Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo Musoma Mkoani
Mara mara baada ya kuwasilia kuzindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu
ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo
Musoma Mkoani Mara kutofanyiana vitendo vya ukatili na kutoa taarifa ya vitendo
hivyo shuleni kabla ya kuzindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili
kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.
Mkuu wa Wilaya ya
Musoma Bw.Vicent Naano akielezea mikakati ya Wilaya katika kupambana
na wale wote watakaosababisha au kuwafanyia wanawake na watoto vitendo vya
ukatili katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili
kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.
Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa USAID akielezea mikakati
ya Serikali ya Marekani kushirikiana na Serikali ya
Tanzania katika mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na
mimba na ndoa za utotoni katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na
walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia shuleni.
Wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Mwisenge iliyopo Wilaya ya Musoma Mkoani Mara wakisikiliza nasaha
kutoka kwa viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mpango wa
mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa
kijinsia shuleni.
Baadhi ya wazazi na wanafunzi
Wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Mwisenge iliyopo Wilaya ya Musoma Mkoani Mara wakisikiliza nasaha
kutoka kwa viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mpango wa
mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo vya ukatili wa
kijinsia shuleni.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
akizindua Mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo
vya ukatili wa kijinsia shuleni katika Shule ya Sekondari Mwisenge iliyopo
Wilaya ya Musoma mkoani Mara.(PICHA NA WAMJW)
NA MWANDISHI WETU- MARA
NAIBU Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
amezindua mpango wa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kupambana na vitendo
vya ukatili wa kijinsia shuleni
Akizungumza katika
uzunduzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika Shule ya Sekondari Mwisenge Dkt.
Ndugulile amesema kuwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia hususani ukatili dhidi
ya wanawake na watoto umeendelea kuwepo chini na takwimu zikionesha mkoa wa
Mara ukiwa na asilimia 32 ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa mimba
na ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa ambapo mkoa wa Mara ni wa tano kitaifa
kwa kuwa na asilimia 37.
“Serikali imeandaa
Mpango wa kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa
mwaka 2017/18-2021/22 na moja kati ya msisitizo katika mpango huu ni kutokomeza
ukatili wa kijinsia shuleni” alisisitiza Dkt. Ndugulile
Aidha Dkt. Ndugulile
amekemea mahusiano ya kingono yaliyopo baina ya walimu na wanafunzi na kuwataka
wanafunzi kuacha kufanyiana vitendo vya ukatili na kutoa taarifa ya vitendo vya
ukatili.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Musoma Dkt.Vicent Naano amesema kuwa wataendelea kupambana na wale
wote watakaosababisha au kuwafanyia wanawake na watoto vitendo vya ukatili.
Pia Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa USAID Bi.Christina Djondo ameihakikishia Serikali ya Tanzania
kuendelea kushirikiana nayo katika mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake
na watoto na mimba na ndoa za utotoni.
Mpango huu wa mafunzo
kwa walimu na wanafunzi utawafikia walimu 1,300 na wanafunzi 26,000.
No comments:
Post a Comment