RAIS wa Jamhuri ya Zimbabwe
Emmerson Mnangagwa alipotembelea chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole
kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani kwa ajili ya ukarabati.
Picha na Mwamvua Mwinyi
……………
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
RAIS wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
ametoa kiasi cho dola elfu kumi kwa mkuu wa chuo cha Kilimo na Mifugo
cha Kaole kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani kwa ajili ya ukarabati.
Ametoa kiasi hicho ikiwa kama shukrani yake ambazo amesema zitasaidia kutatua baadhi ya changamoto chuoni hapo.
Rais Mnangagwa
alisema hayo mapema Juni 29 alipotembelea iliyokuwa shule ya wapigania
uhuru wa chama cha FRELIMO ambacho hivi sasa ni Chuo cha Kilimo na
Mifugo cha Kaole kilichopo Bagamoyo .
Aidha alieleza endapo
kutakuwa na uwezekano ataongeza dola nyingine 50 ili kuongezea kiasi
alichotoa kwa ajili ya ukarabati chuoni humo .
Akiwa chuoni hapo
alisema yeye ni mojawapo ya waanzilishi wa chuo hicho katika miaka ya
sitini akiwa pamoja na viongozi wengine wa Chama cha FRELIMO .
Alisema kwamba
alikuwa kiongozi wa ulinzi wa chuo hicho na hawakuwa na dhumuni la
kutafuta madaraka bali ilikuwa ni jitihada zilizosukumwa na uzalendo wa
kuzipatia nchi zao uhuru.
Rais Mnangagwa
alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwa fursa ya kuitembelea Shule hiyo kwa kuwa ilikuwa ni shauku
yake baada ya kuondoka shuleni hapo miaka 58 iliyopita .
“Nimefarijika
kutembelea Bagamoyo na kuja Tanzania naamini mwaliko huu utaendeleza
mahusiano ya nchi hizi uliokuwepo kipindi kirefu” alibainisha.
Aliwashukuru wananchi
wa eneo hilo kwa kumtunza katika kipindi chote alichoishi Bagamoyo
hata sasa anajisikia kuwa ni mmojawapo wa jamii ya watu wa wilaya hiyo.
Rais huyo aliingia Tanzania Juni 28 ambapo alisema Tanzania na Zimbabwe wataendelea kuimarisha ushirikiano wao .
No comments:
Post a Comment