Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo alipotangaza kuwa kwa mwaka wa tatu mfululizo,
Tigo ndio mdhamini mkuu wa mawasiliano katika Maonesho ya 42 ya
Kimataifa ya Dar es Salaam ya Biashara (DITF) ambayo yanaandaliwa na
Mamlaka ya Ukuzaji wa Biashara Tanzania (Tantrade). Kushoto ni Meneja
wa Ukuzaji wa Biashara wa Tantrade, Stephen Koberou
………………….
Tigo yatoa ofa murwa kwaa simu janja za kisasa zenye vifurushi vya intaneti katika maonesho hayo
Dar es Salaam, Tanzania– Juni 29,
2018: Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo ndio
mdhamini mkuu wa mawasiliano katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar
es Salaam ya Biashara (DITF) ambayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji
wa Biashara Tanzania (Tantrade). Kauli mbiu ya maonesho hayo almaarufu
Sabasaba yanayofanyika
kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2018 ni ‘Ukuzaji
wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda’.
Akitambulisha udhamini huo jijini
Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema
kuwa hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Tigo kudhamini maonesho hayo.
Ushirikiano huu ni sehemu mojawapo ya azma ya Tigo kuchangia juhudi za
serikali kukuza biashara kama njia mojawapo ya kukuza uchumi wa viwanda
nchini.
‘Tigo inatambua kuwa Tanzania ni
mojawapo ya nchi za Afrika ambapo uchumi wake unakua kwa kasi ya juu na
kuwa bado kuna fursa nyingi zinazopatikana nchini. Kila mwaka kwa
kipindi cha miaka 42 sasa, Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya
Biashara (DITF) yamekuwa chachu kubwa ya kukuza uchumi wa viwanda kwani
yanatoa fursa kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa, wadogo na wa kati
kuonesha ubunifu katika bidhaa na huduma, pamoja na teknologia mpya kwa
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Vilevile, Sabasaba ni chachu ya
maendeleo ya kiuchumi kwani inatoa fursa za ajira na mapato kwa sekta
tofauti,’ Woinde alisema.
Aliwahamasisha Watanzania
kujiandaa kupokea ofa kabambe za simu janja za kisasa zenye ofa murua za
vifurushi vya intaneti kwa kipindi cha hadi miezi sita kutoka Tigo.
‘Tumeingia ubia na watengenezaji wakubwa wa simu duniani kama vile
Tecno, Samsung, Nokia na Freetel kuhakikisha kuwa wateja na wananchi
watakaofika katika viwanja vya Sabasaba, Dar es salaam au katika maduka
yote ya Tigo nchi nzima wanafaidika na simu janja kwa bei nafuu kuanzia
TSH 69,000 pekee katika msimu huu wa Sabasaba.’
Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji
wa Biashara wa Tantrade, Stephen Koberou aliwashukuru Tigo kwa kuchukua
jukumu la kuthamini maonesho ya mwaka huu ya Sabasaba ili kukuza
biashara. Pia aliwahamasisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili
waweze kujionea ubunifu na teknologia mpya, kujifunza, kujenga mahusiano
mapya ya kibiashara pamoja na kuwa sehemu ya fursa kubwa zaidi ya
kufanya manunuzi na kupata huduma muhimu kwa bei nafuu.
‘Maandalizi yako tayari na
nawakaribisha wafanyabiashara wote kujitokeza kwa wingi kuunga mkono
wafanyabiashara wenzao wa ndani na nje ya nchi ambao wameleta bidhaa na
huduma zao katika maonesho ya mwaka huu, huku wakipata fursa ya
kujionea hatua kubwa tulizopiga katika kukuza uchumi wa viwanda nchini,’
alisema.
Sabasaba imejizolea umaarufu kama
maonesho yanayoongoza nchini kwa kuvutia mamia ya wafanyabiashara kutoka
ndani na nje ya nchi pamoja na maelfu ya wageni wanaovutiwa na bidhaa
bora na bei nafuu zinazopatikana katika maeonesho hayo.
-MWISHO-
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania www.tigo.co.tz
ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya kidigitali nchini
Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka
1995.
Kupitia huduma zake za kipekee za
sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia
simu za mikononi. Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali. Ni kampuni
ya kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya
Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na kuzindua huduma ya kwanza
iliyowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi
kwenda nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu
ya nchi husika Afrika Mashariki.
Tigo ni kampuni ya simu ya pili
kwa ukubwa nchini na kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, imekuwa
kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kupitia mkakati mkubwa
wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo
ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine
22 nchini.
Tigo inajivunia jumla ya watumiaji
milioni 11 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa
moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao
300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa huduma kwa wateja,
wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa
mauzo na wasambazaji.
Tigo ni nembo ya kibiashara ya
Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya
kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za
kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za
Millicom zipo Ulaya na Marekani.
Kwa taarifa zaidi, wasiliana na: woinde.shisael@tigo.co.tz
No comments:
Post a Comment