Pages

Wednesday, May 2, 2018

VIDEO: SERIKALI YAANDAA KITINI CHA MASUALA YA JINSIA KUENDELEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI WA KITAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE



PIX 1
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mboni Mgaza akielezea dhumuni la Serikali kushirikisha wadau katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18-21/22 kinachofanyika mjini Morogoro.
PIX 2
Mwezeshaji wa Kikao Bw.Clarence Kipobota akitoa mwelekeo wa uendeshaji wa kikao hicho kuhusu masuala ya Jinsia katika mchakato wa kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18-21/22 katika kikao kati ya Serikali na wadau kinachofanyika mjini Morogoro.
PIX 3
Baadhi ya wadau na wataalamu wa masuala ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18-21/22  katika kikao kinachofanyika mjini Morogoro.
Pix 4
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Darius Damas akitoa maoni kuhusu tafiti zinazofanyika na jinsi zinavyoendana na mazingira ya mtanzania katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18-21/22 katika kikao kinachofanyika mjini Morogoro.
Pix 5
Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Zuhura Karya akitoa maoni kwamba kitini kinatakiwa kitoe picha au hali halisi ya mazingira katika eneo husika ili kiweze kueleweka kwa urahisi kwa walengwa.  Hali hii inaweza kuwa kuonyesha sinema na picha. Hayo yalizungumzwa na Bi Zuhura Karya katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18-21/22 katika kikao kinachofanyika mjini Morogoro.
Pix 6 (1) Pix 6
Baadhi ya wadau na wataalamu wa masuala ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakijadiliana katika makundi  katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18-21/22  katika kikao kinachofanyika mjini Morogoro.
 Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
 …………………………
Na Mwandishi Wetu – Morogoro
Serikali kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto imeanza mchakato wa kuandaa kitini cha masuala ya Jinsia kuendeleza kasi ya utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Akizungumza katika kikao cha wataalam na wadau wa Maendeleo ya Jinsia Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza amesema kuwa Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto umekithiri sana nchini na hivyo Serikali kuamua kutafuta njia tofauti za kupambana na tatizo hilo.
Ameongeza kuwa lengo la kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module”ni kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambao utatoa uelewa kwa wadau wa maswala ya jinsia na maafisa Maendeleo ya Jamii kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri na kata ili kutoa elimu ya masuala ya Jinsia katika jamii.
Bi. Mboni amefafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya wanawake nchini ilikuwa ni 23,058,933 sawa na asilimia 51.3 ya watanzania na ndio wanaokumbwa na vitendo vya ukatili kwa kiasi kikubwa
Amesisitiza kuwa kitini hicho kitazingatia masuala mbalimbali kama vile lugha na mazingira ya walengwa hasa wa vijijini ili kiweze kuleta matokeo mazuri katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.
“ Naamini mara baada ya majadiliano haya tutatoka na kitini kitakachotuongoza katika kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.” Alisema Bi. Mboni.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Zuhura Karya ameomba kitini hicho kielekeza zaidi kuwasaidia wanawake na watoto wanaokumbwa na vitendo vya ukatili katika maeneo ya vijijini ambapo wengi wao hawana wa kuwasemea.  
Wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia wamedhamilia  kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watotowa mwaka  2017/18-21/22 nchini.

No comments:

Post a Comment