Na Mahmoud Ahmad Dodoma
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, sanaa na
Michezo, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
Kilele cha Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini .
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma , Katibu wa Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF) Nevile Meena alisema mada mbalimbali zitakazojadiliwa ni
pamoja na changamoto zinazovikumba vyombo vya habari katika kipindi cha
miaka 27 tangu Azimio la Windhoek, Namibia, lilipopitishwa linalohusu
uhuru wa vyombo vya habari.
Akieleza
zaidi alisema, Kilele cha Maadhimisho hayo kitafikiwa kesho, Mei
3, mwaka huu, mkoani Dodoma, ambapo siku moja kabla kutakuwa na
majadiliano kuhusu hali ya vyombo vya habari nchini ambayo yatafunguliwa
na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
“Tutapata
Wakati muafaka wa kujadili mada kuu ya changamoto zetu, pia kutakuwa na
mada nyingine zitakuwa zinaendelea katika vikundi, ikiwemo inayohusu
mitandao ya kijamii kama inatakiwa kudhibitiwa au watumiaji ndio
wajidhibiti wenyewe,” alisema Meena.
Pamoja
na hayo alisema kutakuwa na mada kuhusu unyanyasaji wa kingono ndani ya
vyombo vya habari, na kuona kama suala hilo bado ni kikwazo hasa kwa
waandishi wanawake kupata nafasi za juu kwenye vyombo vya habari.
Aidha
Katibu huyo wa TEF alisema, kutakuwa na mada kuhusu usalama wa
waandishi wa habari, ni kiasi gani waandishi wanakuwa salama wanapofanya
kazi zao katika maeneo mbalimbali.
“Suala
la haki za kupata habari, japo limeingizwa kwenye sheria tangu mwaka
2016 na kanuni zake Februari mwaka huu, na namna gani mwandishi anaweza
kudai haki hiyo,” alisema.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Klabu za Waandishi Tanzania (UTPC), Jane Mihanzi
aliyataja maadhimisho hayo kuwa ni fursa kwa wadau wa habari kujadili
namna vyombo vya habari vilikotoka, vilipo na wapi vinaelekea.
”
Sisi kama wadau wa habari tunaotambua na kuwajali wananchi kupata
habari, tumekuwa tukisaidia waandishi kuwapamafunzo na vifaa vya
kazi,”alisema.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Razia
Mwawanga alisema kupitia maadhimisho hayo wanahabari na jamii kwa ujumla
wataelewa umuhimu na wajibu wa kuwajibika.
Alisema,japo
kuwa taaluma hii ina vikwazo vingi kuna ,waandishi watapaswakuwajibika
kwa kujitolea ikiwa ni pamoja na kuhamasika kuacha kuandika habari kwa
mazoea na bafala yake wajikite katika kuandika habari zenye maslahi za
kueleza wajibu wa serikali kwa umma na umma kwa serikali yao.
Hata hivyo alisema fani ya uandishi habari inapaswa kujikita katika
maadili ya uandishi bora kwa kuzingatia vigezo weledi na si vinginevyo
kwani hii itasaidia ukuwaji wa fani hiyo hapa nchini na kuondokana na
uandishi wa kimazoea katika kutekeleza majukumu ya wanahabari ya kila
siku.
No comments:
Post a Comment