……………
Katika kusherehekea siku ya
Wafanyakazi Duniani, wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameungana na
wafanyakazi wote Duniani kwa kujumuika na wafanyakazi wengine wa hapa
nchini jijini Dodoma na kuahidi kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi kwa
Watanzania.
Wakiongea kwa nyakati tofauti
wakati wa sherehe hizo wafanyakazi hao, wamesema kuwa ofisi ya Waziri
Mkuu kama mratibu wa shughuli zote za serikali nchini na kama mratibu wa
shughuli za Kazi na ajira nchini wataendelea kutekeleza majikumu hayo
kwa uadilifu na ufanisi ili huduma zinazotolewa na serkali ziwe zenye
tija kwa Watanzania.
Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na
kuratibu Shughuli zote za serikali ndani na nje ya Bunge pia inaratibu
masuala mtambuka, kama shughuliza maafa, Udhibiti wa matumizi ya madawa
ya Kulevya, Vita dhidi ya UKIMWI, Huduma kwa watu wenye Ulemavu. Aidha
inahusika na kuchapa nyaraka za uendesheshaji shughuli za serikali,
masuala ya Vyama vya siasa, Masuala ya Uchaguzi, Masuala ya kazi, Ajira
na maendeleo ya vijana, pamoja na masuala ya uwekezaji na uwezeshaji
wananchi kiuchumi.
Maadhimisho ya sherehe za siku ya
Wafanyakazi Duniani mwaka huu zimebebwana kauli mbiu ya “Uunganishaji wa
Mifuko ya Jamii ulenge kuboresha mafao ya mfanyakazi”
No comments:
Post a Comment