Pages

Sunday, April 1, 2018

CHONDE CHONDE MAASKOFU MSISOME KESHO WARAKA WENU PIGINE MAGOTI TUOMBEENI – MBUNGE RITTA KABATI



 Na  MatukiodaimaBlog
WAKATI  kesho makanisa  mbali  mbali ya kikristo nchini yanatarajia
kutumia ibada ya sikukuu ya Pasaka ambayo ni maalum  kwa  ajili ya
kumbukumbu ya  kufufuka kwa  Yesu Kristo ,kusoma  waraka maalum  kwa
Taifa , mbunge  wa  viti  maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM)
amewaomba maaskofu nchini  kusitisha kusoma  waraka  huo na badala
yake  kupiga magoti  kuliombea Taifa.
 
Kuwa
kila  mmoja anapokea  tofauti matamko  hayo  hivyo  wanaweza  kusema
wanafanya  kwa utume wa  Mungu  kumbe  wakavuruga  utume  wa Mungu
kupitia matamko  hayo makanisani ni  vema  wakapiga magoti ya  kusali
sio  kusoma  waraka  huo  wasome Biblia kusherekea  kufufuka kwa Yesu
kristo.
 
Akizungumza leo   na  wanahabari
wakati  zoezi  fupi na ofisi ya  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza
kuwaongoza  wananchi wa  mji wa Iringa kukabidhi  misaada mbali mbali
ikiwemo ya  nguo na chakula kwa watoto  yatima  wa  kituo cha
Tosamaganga ,mbunge Kabati  alisema  kuwa waraka  huo wa maaskofu
umezua   hofu  kubwa kwa  wananchi na kila mmoja kutaka  kuusikia  japo
aliomba hekima  ya maaskofu  kutumika katika suala  hilo .
 

Sio  kwamba nawapangia majukumu ya kufanya  maaskofu  na  viongozi
wangu wa  dini ila naomba zoezi hili la  waraka  kusitishwa  kusoma
makanisani na badala yake viongozi hao  wa  dini kufanya kazi ya
kuliombea  Taifa na  watu wake badala ya  kutoa  waraka”
 
Kabati
alisema  kuwa  jukumu  kubwa la  viongozi wa  dini  ni kueneza  injili
na watu  wakakombolewa  kupitia  injili na  sio  kuwafanya  watu  kuwa
na  hofu kama  iliyowekwa na viongozi hao wa dini  kupitia waraka   huo
ambao haujulikani una nini ndani yake kwa Taifa kwani ni  waraka ambao
umekuja ghafla  umeanza  kuzua mgawanyiko  hata  miongoni mwa dhehebu
moja  hadi jingine na askofu  mmoja  na mwingine jambo ambalo  si
sahihi .
Mbunge  huyo  alisema  ingependeza
kwa  maaskofu hao na  viongozi  wengine wa  dini za  kikristo  kwa
wakati  huo  wa  Pasaka ambao ni  wakati kusherekea  kufukuka kwa  Yesu
Kristo na  wakati wa ule  wa  mateso ya  Yesu  wangejielekeza  zaidi
katika  kuzama katika maombi ya kuliombea  Taifa  ili  waumini  wao
wafanye kazi za  kusambaza  upendo na  kuwasaidia  watu  wenye mahitaji
kama yatima na  wengine  waliokosa faraja  kuliko kuwaandaa kuujua
waraka  huo .
 
” Tayari  baadhi ya makanisa
wamekwisha toa waraka  ambao  pamoja  na kuwa  walidai ni waraka mwema
ili  umeonekana ni  waraka  wa mlengo furani ambao unawagawa hata
waumini  wao ambao wapo  upande  ambao  wao wanauunga  mkono chonde
chonde viongozi wa dini ni  vizuri  kuwaelekeza waumini wenu  kuyajua
maandiko na kuomba kwa ajili ya wenye shida  kuliko kukimbilia  kutoa
waraka  hata  Biblia  imesema ya Kaisali mwachie  Kaisali na ya  Mungu
mwachia Mungu sasa badala ya  kutoa matamko  wao  wangetuombea  haya
matamko yanapokelewa  tofauti “
Hata  hivyo
mbunge  huyo  alimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Mazenza kwa hatua ya
kuwaunganisha  pamoja wadau mbali mbali na  wananchi wa mji wa Iringa
kwenda  kusaidia watoto  yatima  Tosamaganga  na  kuwa utamaduni  huo
unapaswa  kuwa  endelevu katika  sikukuu zote za kikristo na kiislamu
kwani umeanza  vizuri .
 
Kwa  upande  wake  mkuu
wa  mkoa wa Iringa Masenza  mbali ya  kuwapongeza wananchi  mbali
mbali  na  viongozi wa CCM na serikali  na  wafanyabiashara  mkoani
hapo  kujitokeza  kuungana kwenda kusaidia  yatima  hao bado  alisema
suala la upendo linahitajika  kuwa endelevu na  kuwa   ofisi yake
imelazimika kuratibu  zoezi hilo la kwenda kusaidia yatima  ili
kuwafanya nao washerekee Pasaka kama watoto  walio na wazazi wao .
 
Alisema
pamoja  na  vitu  mbali mbali ambavyo  vimechangwa kwa  ajili ya
watoto hao  pia kuna mbuzi ,mafuta na  kula ,nguo ,sabuni ,pipi toka
Ivori  pamoja na pesa kiasi cha  zaidi ya  shilingi 450,000 zilizotolewa
na  wadau hao kwa ajili ya watoto hao .
 
Aidha
mkuu huyo wa  mkoa alitaka  wananchi  wa mkoa wa Iringa kusherekea
sikukuu  hiyo kwa amani na utulivu na kuwa ofisi yake  kupitia  vyombo
vya ulinzi na usalama na  vyombo  vya sheria  hataacha kuchukua hatua
kali kwa  mwanaume  yeyote  atakaye lewa  pombe na  kumpiga mke wake
wakati wa sikukuu.

No comments:

Post a Comment