Mwingereza Anthony Joshua amefikisha mikanda mitatu ya uzito wa juu baada ya kumtwanga Joseph Parker kwa point.
Pambano la wakali hao wawili lilikuwa la kuvutia na kusisimua likiwa na ushindani kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Hata hivyo Joshua
alifanikiwa kuongoza kwa raundi na Paker raia wa New Zealand mara kadhaa
hasa raundi ya sita alijitahidi kujitutumua.
Mashabiki 80,000
walikuwa ukumbini wakati Joshua akishinda taji la WBO na sasa kuwa na
matatu jumla maana anao yale ya IBF na WBA.
No comments:
Post a Comment