Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (aliyesimama)
akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua programu ya wanafunzi walimu kutoka
Chuo Kikuu cga Dodoma wanaokwenda kujitolea kwenye shule za Sekondari
na Msingi zilizo karibu na maeneo wanayoishi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Dodoma Mhe.Davis Mwamfupe akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kuzindua program ya wanafunzi walimu wa UDOM wanaokwenda kujitolea
kwenye Shule za Msingi na Sekondari.
Mratibu wa program ya kujitolea
kwa Wanafunzi Walimu Dr.Ombeni Msuya ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Dodoma akielelezea namna walivyojipanga kusimamia program
hiyo.
Mwenyekiti wa Wanafunzi Walimu
wanaokwenda kujitolea akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu hiyo
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga iliyopo Mjini
Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi walimu wa
Chuo Kikuu cha Dodoma wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kabla ya
uzinduzi wa program maalumu ya kwenda kujitolea kwenye Shule za msingi
na sekondari.
………………………………………………………………………………………………
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dodoma wanaosomea Shahada ya Ualimu wameunga mkono jitihada za Serikali
ya Awamu ya Tano katika Utoaji wa Elimu Msingi bila malipo kwa
kujitolea kwenda kufundisha katika shule za msingi na Sekondari zilizoko
katika maeneo yao wakati wa Likizo.
Akizindua mpango huo wa kujitolea
kwa wanafunzi walimu zaidi ya 500 Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka wanafunzi hao
kuwa mfano ya kuigwa kwenye shule watakazoenda kufundisha ili kuipa
heshima zaidi programu hii iweze kuwavutia walimu wengine zaidi.
Alisema kuwa mnapofika mashuleni
mkawe mfano bora kwa wadogo zenu, mkaonyeshe uwezo wenu katika
kufundisha na kuwafikishia yale muhimu katika masomo yao, mkaonyeshe
Umahiri katika Taaluma yenu ndipo kujitoa kwenu kutaheshimiwa na
kuthaminiwa na jamii nzima ya watanzania.
Aliongeza kuwawanafunzi wa UDOM
mnaokwenda kujitolea ndio mtakua waasisi wa programu hii kitaifa hakuna
eneo lolote Nchini ambako wanafunzi walimu kwa Umoja wao waliamua kwa
hiari kwenda kufanya kazi katika jamii walizotoka tena bila malipo
yeyote kwa wengine watakaofanya hivi katika maeneo yao watakua wameiga
kutoka kwenu.
“Huu ni Uzalendo wa hali ya juu
na mmejitoa kwa Taifa lenu na kupitia kujitolea kwenu mnasaidia kutatua
changamoto zinazokabili Wizara ya TAMISEMI hakika mnapaswa kutambuliwa
na kuweka kumbukumbu sahihi ya nani na nani alishiriki katika program
hii” Alisema Jafo.
Akizungumza katika Uzinduzi wa
kampeni hiyo Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe.Prof.Davis Mwanfupe amewaasa
wanafunzi walimu wanaokwenda kujitolea na kuwakumbusha kwenda kuitumia
vyema Taaluma yao kwa kuwa Nuru ya kuiangazia jamii katika mambo yale
yaliyo mema.
Naye Mratibu wa Programu hii
ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma Dr.Ombeni Msuya amesema
huu ni muendelezo wakampeni ya Nipe Daftari na Peni, Nami nipate Elimu
iliyozinduliwa na Waziri Jafo hivi karibuni.
Amesema sababu ya programu hii
inatokana na ukweli kwamba shule nyingi za Serikali zina Upungufu wa
Walimu kutokana na Upatikanaji wa Elimu bure ambao umeongeza Idadi ya
wanafunzi katika shule nyingi kuanzia Msingi hadi Sekondari hivyo
wakaona ni vyema kuratibu wanafunzi walimu waweze kwenda kuunga Mkono
jitihada hizi za Serikali.
Hata hivyo Dr. Abdallah Seni
ambaye pia ni miongoni mwa waratibu wa Programu hii alisema sisi ni
sehemu ya wanataaluma na wataalamu, kwa pamoja tumeazimia kuhamasisha
walimu wanafunzi na walimu wengine wanaofanya kazi nje ya Ualimu,
kuitikia wito wa kujitolea kufundisha katika shule ambazo wapo jirani
nazo kama sehemu ya uzalendo na upendo kwa Nchi yao.
No comments:
Post a Comment