WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekagua mradi wa usambazaji wa maji kwenye vijiji vinavyopitiwa na
mradi wa maji Mbwinji na ameridhishwa na unavyoendelea.
Mradi huo unaosimamiwa na
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA)
unatarajiwa kukamilika Machi 31, 2018.
Waziri Mkuu alifanya ukaguzi huo
jana (Alhamisi, Machi 01, 2018) katika kioksi cha kuchotea maji
kilichopo kwenye kijiji cha Mbecha wilayani Ruangwa.
“Huduma ya upatikanaji wa maji
safi na salama kwa wananchi ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya
Awamu ya Tano, hivyo vijiji vyote vitapata maji”.
Waziri Mkuu alisema vijiji
ambavyo vimenufaika na mradi huo wilayani Ruangwa ni sita ambavyo ni
Chiyapi, Nandanga, Ipingo, Lucheregwa, Litama na Mbecha.
Alisema Serikali ya Awamu ya
Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa
maji safi na salama katika maeneo yote yenye ctatizo hilo nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mtendaji wa MANAWASA Mhandisi David Mwamsojo alisema mradi huo
utagharimu sh. milioni 870.738 hadi kukamilika.
Alisema mradi huo unahusisha
vijiji 12 vilivyo kwenye umbali wa kilomita tano kutoka kwenye bomba kuu
pamoja na ujenzi wa vioksi 18 vya kuchotea maji.
Mhandisi Mwamsojo alisema hadi
sasa tayari kazi ya ulazaji mabomba na kuweka vituo 16 vya kuchotea maji
katika vijiji 11 vinavyonufaika na mradi huo imekamilika na wananchi
wanaendelea kupata huduma ya maji.
Alitaja vijiji hivyo kuwa ni
Mtepeche, Magereza, Mailisita, Mkotokuyana na Naipanga vya wilaya ya
Nanchingwe na Chiyapi, Nandanga, Ipingo, Lucheregwa, Litama na Mbecha
vya wilaya ya Ruangwa
No comments:
Post a Comment