Mama Josephine Bakhita akiwa na
watoto wenye ulemavu wa viongo na akili. Watoto hao ni wa familia moja
ya Mzee Semgweno, wanaoishi katika kijiji Cha Mvomero, Kata na Tafara ya
Mvomero, Wilani Mvomero mkoni Morogoro. Mama Josephine Bakhita kupitia
Taasisi yake ya
EMFERD amekuwa akisaidia familia hiyo kupata mahitaji
mbali mbali japo uwezo wa taasisi ya EMFERD haukidhi mahitaji ya familia
hiyo na walemavu wengine wanaolelewa na taasisi hiyo.
Picha na Mpiga EMFERD.
……………….
Na Mwandishi wa EMFERD
Jamii pote nchini imeombwa
kuwasaidia wasiojiweza katika msimu huu wa sikukuu ili wasiojiweza nao
wajihisi kama ni sehemu ya jamii hiyo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Erick inayotoa elimu na Marekebisho kwa
Wenye Ulemavu (EMFERD) Josephine Bakhita kijijini Mvemoro Wilayani
Mvomero mkoani Morogoro jana.
Bakhita alisema kuwa jamii za
walemavu, yatima, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ni
vema zikawa zinakumbukwa misimu ya sikuu kwani nao wanahitaji kufurahi
pamoja na wana jamii wengine.
“ Wapo watoto wenye ulemavu wa
viungo na akili, wapo watoto yatima, wapo wafungwa, wagonjwa wapo wazee,
wapo wafungwa katika kipindi hiki cha Pasaka ni muhimu sana jamii hizi
zikakumbukwa ili nazo zisijihizi kutengwa na wanajamii wenzao” Alisema
Bakhita.
Aliongeza kusema kuwa baadhi ya
familia zinakula vizuri na kuvaa vizuri, zipo familia ambazo zinasaza
vyakula na hata kutupa jalalani ama kutumia vileo, basi ni vema kwa
taasisi, mashirika na watu binafsi kuyafikiria makundi ambayo yamepoteza
matumaini na hayana uwezo wa kupata hata mlo mmoja kwa kuwapatia
chochote kitu iwe ni mavazi au vyakula kwa lengo la kuzifanya jamii hizo
kufurahi na kutohisi kutengwa.
No comments:
Post a Comment