Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani akikagua moja ya maeneo ya mashamba ya wanna vijijini
zitakapopitaa nguzo za kusafisha umeme wa REA III.
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (katikati) akigawa bure kifaa cha umeme tayari(UMETA) kwa wazee
8 ambapo wanne wanatoka Kijijiji cha Miguha Wilayani Nzega na na
wengine 4 kutoka Kijiji cha Matinje Wilayani Igunga mkoani Tabora ikiwa
Ni ishara ya kuwahamasisha Wananchi wengine kununua vifaa hivyo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (katikati) akigawa bure kifaa cha umeme tayari(UMETA) kwa wazee
8 ambapo wanne wanatoka Kijijiji cha Miguha Wilayani Nzega na na
wengine 4 kutoka Kijiji cha Matinje Wilayani Igunga mkoani Tabora ikiwa
Ni ishara ya kuwahamasisha Wananchi wengine kununua vifaa hivyo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (kushoto) akiteta Jambo na mbunge wa Manonga katika Kijiji cha
Matinje baada ya kukagua Mradi wa REA III, katika wilaya ya Igunga
mkoani Tabora.
……………….
Na Zuena Msuya Tabora,
Halimashauri za Wilaya nchini
zimeshauriwa kutenga fedha kwa ajili ya kuziunganishia Taasisi za umma
huduma ya umeme ya umeme unaotokana na Mradi wa kusambaza wa umeme
Vijijini REA Awamu ya Tatu.
Ushauri huo ulitolewa na Waziri wa
Nishati Dkt.Medard Kalemani wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kukagua
maendeleo ya utekelezaji wa Mradi REA III katika Kijiji cha Miguha
Wilayani Nzega na kijiji cha Matinje wilayani Igunga mkoani Tabora.
Dkt. Kalemani alisema kuwa licha
ya Taasisi za umma kupewa kipaumbele katika kuunganishwa na huduma za
umeme lakini halmashauri nyingi zimekuwa hasitengi fedha wala kutandaza
nyaya katika Taasisi hizo zilizopotiwa na Mradi wa REA III na
kusababisha changamoto katika kutekeleza mradi huo pamoja kuwaleta adha
wananchi.
Alisisitiza kuwa ni vyema
halmashauri zikatumia fursa ya umeme wa REA katika kuziungasha Taasisi
za Umma kwa kuwa huduma ya umeme huo hupatikana kwa bei nafuu zaidi
tofauti na kuunganishwa kwa gharama za Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) .
” Mradi wa REA unapita katika kila
Kijiji, Halmashauri zote zinafahamu hili cha ajabu hasitengi fedha kwa
hiyo Shule, hospitali na Taasisi zote zinazotoa huduma kwa jamii
haziunganishwi na huduma ya umeme, halmashauri tengeni fedha wananachi
wapate huduma Bora na kisasa”, alisema Kalemani.
Aliwasisiza Wananchi hasa wasio na
nyumba zinazohitaji wiring kuchangamkia fursa ya mradi wa Umeme
Vijijini REA III, kwa kutumia kifaa cha Umeme tayari (UMETA)
kitakachopatikana bure kwa wateja 200 wa mwanzo watakaolipia na
kuunganishwa na huduma ya umeme.
Katika ziara hiyo Dkt. Kalemani
alisema kuwa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu nguzo za zege zitaanza
kutumika ili kumaliza tatizo la kudondoka kwa nguzo zilizochakaa au
kuchomwa Moto wakati wa kuandaa msimu wa kilimo.
Aliweka wazi kuwa nguzo hizo
zitatengezwa hapahapa nchini ambapo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
litakuwa na kiwanda cha kutengeneza nguzo hizo pia wawekaji wa ndani na
nje wanaalikwa kuanzisha viwanda vyao nchini.
“Nguzo yoyote ya umeme
itakayoanguka iwe kwa upepo,kuoza au kuchomwa Moto kuanzia mwezi
Septemba mwaka huu mbadala wake itasimamishwa nguzo ya zege hizo
zitamaliza kabisa tatizo la nguzo kuangua Mara kwa Mara, nguzo hizi za
zege zinadumu muda mrefu japo zinatengezwa kwa gharama kubwa”,
alisisitiza Dkt.Kalemani.
Katika hatua nyingine DKt.Kalemani
amewaalika wawekazi wa nje na ndani kuwekeza katika mkoani Tabora kwa
kuwa Mkoa huo una Nishati ya umeme ya kutosha na ziada ambayo wakazi
wake hawawezi kuitumia yote.
Alisisitiza kuwa ni marufuku kwa
mkoa huo kuwa na tatizo la Kukatikakatika umeme na endapo itatokea Basi
Wananchi waelezwe Nini kimesababisha.
No comments:
Post a Comment