Na Mwandishi wetu
Madaktari Bingwa wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na
Madaktari wa Hosipitali ya BLK India leo wamefanya upasuaji maalum wa
mgongo kwa kutumia matundu (Minimal Invasive Spine Surgery) kwa mgonjwa
aliyedhoofika uti wa mgongo.
Kwa Mujibu wa Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Taasisi hiyo Jijini Dar es
Salaam, Upasuaji huo umefanywa kwa mafanikio makubwa ukiwashirikisha
Madakatari Bingwa wanne wakiongozwa na Profesa Joseph Kahamba wa MOI na
Dkt. Puneet Girdhan kutoka hosipitali ya BLK.
Taarifa hiyo imebainisha
kuwa upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa kwa
muda wa masaa
manne ambapo pamoja na upasuaji huo, MOI imeanzisha huduma za upasuaji
wa magoti kwa njia ya matundu ( Athroscopy ).
“ Tayari wagonjwa 300
wameshafanyiwa upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu kwa ufanisi mkubwa
na wagonjwa wengine wameendelea kunufaika na huduma hii” Inasisitiza
sehemu ya Taarifa hiyo
Kutokana na mabadiliko
ya teknolojia ya matibabu, upasuaji wa kupanua njia za mishipa ya fahamu
na kuimarisha uti wa mgongo kwa nyenzo za kisasa umeshika hatamu na
Taasisi hiyo imeendelea kufanya mabadiliko ili kuendana na hali hiyo.
Taasisi ya MOI na
Hospitali ya BLK ya India zilianzisha ushirikiano mwaka 2016 na hii ni
mara ya pili kwa wataalamu kutoka hosipitali hizi kufanya upasuaji kwa
kushirikiana.
No comments:
Post a Comment