Waziri wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.
…………..
Wizara
ya Maliasili na Utalii ya Tanzania Bara na Wizara ya Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar zimeweka mkakati wa pamoja wa kuimarisha
ushirikiano wa usimamizi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii kwa
maslahi ya pande zote za Muungano.
Hayo
yameelezwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi baada ya mkutano wa pamoja wa wizara hizo uliofanyika
hivi karibuni katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.
hivi karibuni katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.
Mkutano
huo wa siku moja uliongozwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Joseph
Meza.
Akifungua
Mkutano huo wa siku moja, Maj. Gen. Milanzi alisema pamoja na Wizara
hizo kutokuwa za muungano imekuepo haja kubwa ya kukutana kwa ajili
kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha sekta ya maliasili
na utalii na kukabiliana na changamoto zinazogusa sekta hiyo katika
Muungano.
“Tumejadiliana
kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya
biashara ya mazao ya misitu, biashara ya Wanyamapori inayohusiana na
mikataba ya CITES na mikataba mingine ya ndani na ya Kimataifa.
“Tumekubaliana
pia kuhuisha sheria zinazokinzana katika usimamizi wa sekta
tunazozisimamia ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza katika
utekekezaji na hivyo kuathiri Muungano wetu,” alisema Maj. Gen.
Milanzi.
Alisema
katika mkutano huo wa siku moja wataalamu kutoka pande zote za Muungano
waliagizwa kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendesha biashara
ya mazao ya misitu na kupendekeza utaratibu wa kufanya biashara kwa
kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo.
Alisema
kupitia mkutano huo Wizara hizo zimeunda kamati maalum ya kuratibu
utekelezaji wa maazimio ya pamoja ya kuimarisha usimamizi bora wa sekta
hizo na utatuzi wa changamoto zilizopo kwa kuandaa mapendekezo ya
kimkakati ya muda mfupi na mrefu.
“Kamati
hiyo itaongozwa na Afisa Mipango Mkuu Msaidizi kutoka Idara ya Misitu
na Maliasili Zisizorejesheka (DFNR), Saleh Kombo Khiari na Mchumi kutoka
Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii, Mugure
Wambura,” alisema Milanzi.
No comments:
Post a Comment