Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo
mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano
wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es
salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo
kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga
saratani ya mlango wa kizazi
Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo
Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni
rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya
kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau
akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya
kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akiteta jambo na
Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi
Wadau wa Afya na Waandishi wa
Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha)
wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa
kizazi
Picha ya pamoja ikiongozwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu (MB) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga
saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
…………………..
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na
Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia
umri wa miaka 9 mpaka 14 huku lengo likiwa ni kuondoa tatizo hilo
nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB)
mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya
kukinga
saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
“Katika kukabiliana na ugonjwa wa
Saratani na kuimarisha afya ya wanawake Tanzania na kupunguza vifo
vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya
kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi”. Alisema Mhe.
Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa
kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Ocean Road Saratani ya Mlango wa
kizazi zinazoongoza nchini kwa Asilimia 36 huku ikifuatia na saratani ya
matiti, huku jumla ya wagonjwa wa Saratani nchini katika kila wagonjwa
100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya
Matiti.
Aidhe, Serikali imepanga kuanza na
wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri wa chini, huku ikitegemea
kuchanja zaidi ya wasichana 610,000 katika jitihada za kutokomeza kabisa
tatizo hili la Saratani ya mlango wa kizazi nchini,
Mhe Ummy alisisitiza kuwa Chanjo
hii itatolewa katika vituo vyote vya Afya nchini vya Serikali, vya watu
binafsi na vikundi mkoba bure, na kuwahimiza wazazi na walezi
kuhakikisha mabinti zao wanapata chanjo hii ili kujikinga na ugonjwa
huo.
Nae Meneja wa Mpango wa Taifa wa
Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Dafrossa Lyimo aliendelea kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza juu ya
umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na
imethibitishwa na shirika la Afya duniani na mamlaka ya chakula na
viodozi nchini (TFDA).
No comments:
Post a Comment