Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard
Kalemani (kulia)akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa shinyanga Zainabu
Tellack wakati wa warsa ya wadau wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi
kutoka Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania uliofanyika
wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard
Kalemani (wa tatu kulia waliokaa) na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Wiliam Lukuvi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali wa Wilaya ya Kaham mkoa wa shinyanga wakati wa warsa ya wadau
wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi bandari
ya Tanga Tanzania uliofanyika mkoani
Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard
Kalemani( wa pili),waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam
Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Tellack wakati warsa ya
wadau wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi
bandari ya Tanga Tanzania uliofanyika mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati,
Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Nishati na
Maendeleo ya Petroli Mhandisi Innocent Luoga( kushoto) wakizungumza na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela( katikati) nje ya
ukumbi wakati warsa ya wadau wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka
Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania uliofanyika mkoani
Shinyanga
……………….
Wakazi wa Shinyanga watakiwa changamkia fursa za ajira
Na Zuena Msuya Kahama, Shinyanga,
Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard
Kalemani amesema kiwanda kikubwa cha kusanifu mabomba yatakayotumika
katika ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka
Hoima nchini
uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania kitajengwa katika
mji wa Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga .
Vile vile alieleza kuwa Wilaya ya
Kahama ni miongoni mwa Wilaya 24 nchini zitakazopitiwa na Mradi wa
Ujenzi wa Bomba hilo la kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini Uganda
hadi Tanzania .
Kufuatia ujenzi wa kiwanda hicho
pamoja na utekelezaji wa mradi wa bomba, Dkt Kalemani aliwataka wakazi
wa Mkoa wa Shinyanga kuchangamkia fursa za ajira kwa kuwa zitatoa
kipaumbele kwa watanzania.
Dkt. Kalemani alisema hayo wakati
wa Warsha ya Wadau wa Bomba la Kusafirisha Mafuta ghafi Afrika
Mashariki iliyofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga,kwa lengo la
kutoa elimu na kueleza hatua iliyofikiwa katika maendeleo ya utekelezaji
wa mradi.
Akizungumzia suala la ajira, Dkt.
Kalemani alifafanua kuwa zaidi fursa ya ajira na ajira elfu kumi(
10,000) zitapatikana wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba
hilo ambazo zitatoa kipaumbele kwa watanzania wenye sifa na taaluma
husika pia kwa wale wasio na taaluma kwa kuwa kuna kazi nyingine
zisizohitaji taaluma.
” Wakazi wa Kahama changamkieni
fursa za ajira na shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato, sitarajii
kuona watanzania wakikosa ajira,kazi zitakuwa nyingi sana kwa wenye sifa
na wasio na sifa, tijitume na tuwe wabunifu zaidi mradi huu ni kwa
manufaa yetu sisi,” alisisitiza Dkt. Kalemani
Aidha alisema kuwa kuwepo kwa
mradi huo kuitaingizia Serikali mapato yatokanayo shughuli mbalimbali za
kibiashara zitakazo kuwa zikifanyika katika eneo hilo.
Kuhusu hatua iliyofikiwa katika
maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, Dkt. Kalemani alisema kuwa ujenzi
rasmi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi unatarajiwa utaanza
mwezi Mei mwaka huu na kwa sasa kinachoanyika ni kuchukuwa sampuli ya
tathmini ya namna ya ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopitia na mradi
huo.
“tone la kwanza la mafuta
litadondoka 2020, huu ni uwekezaji mkubwa sana, tuipondeze serikali ya
awamu ya tano kwa kuhakikisha mradi huu unakuja Tanzania, nchi nyingi
ziliuhitaji, wananchi tuunze na kuulinda mradi wetu”, alisisitiza Dkt.
Kalemani.
Bomba hilo lenye urefu wa kilometa
1443 litajengwa kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na linatarajiwa
kukamilika ifikapo mwaka 2020 litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa
216,000 kwa siku.
Katika hatua Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu aliwataka wanawake kuchangamkia fursa ya ajira na
biashara katika mradi huo wa bomba kwa kuwa wanawake wengi
wamekuwakibaki nyuma.
hivyo amewaasa viongozi hasa wale
wanawake kutoa hamasa kwa wanawake wote ambapo maeneo yatapitiwa na
bomba la mafuta kufanya kila jitihada ili waweze kunufaika kiuchumi
kupitia mradi huo kwa kufanya shughili mbalimbali ikiwemo biashara
ndogo.
No comments:
Post a Comment