Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ,Wiliam Lukuvi, akizungumza wakati wa Warsha ya
Wadau wa Bomba la kusafirisha Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda
Hadi katika bandari ya Tanga nchini uliofanyika wilayani Kahama,mkoani
Shinyanga kwa Lengo la kutoa elimu juu ya mradi wa bomba Hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ,Wiliam Lukuvi (katika), Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani (kushoto) na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(kulia)
wakati wa Warsha ya Wadau wa Bomba la kusafirisha Mafuta ghafi kutoka
Hoima nchini Uganda Hadi katika bandari ya Tanga nchini uliofanyika
wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa Lengo la kutoa elimu juu ya mradi
wa bomba Hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ,Wiliam Lukuvi (kulia) akiwasili katika Warsha ya
Bomba la kusafirisha Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda Hadi
katika bandari ya Tanga nchini uliofanyika wilayani Kahama,mkoani
Shinyanga kwa Lengo la kutoa elimu juu ya mradi wa bomba Hilo.
Baadhi ya wadau wa Warsha ya Bomba
la kusafirisha Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda Hadi katika
bandari ya Tanga nchini uliofanyika wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa
Lengo la kutoa elimu juu ya mradi wa bomba Hilo.
……………………..
Na Zuena Msuya, Kahama Shinyanga.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ,Wiliam Lukuvi amewapiga marufuku wananchi wenye
tabia ya kuvamia maeneo yanayopitiwa na miradi mikubwa ya maendeleo kwa
Lengo la kulipwa fidia ikiwemo Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi kutoka hoima nchini uganda hadi Bandari ya Tanga nchini
Tanzania.
Lukuvi aliyasema hayo wakati
akizungumza katika Warsha ya Wadau wa Bomba la
kusafirisha Mafuta ghafi
kutoka Hoima nchini Uganda Hadi katika bandari ya Tanga nchini
uliofanyika wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa Lengo la kutoa elimu
juu ya mradi wa bomba Hilo.
Alifafanua kuwa baadhi ya wananchi
wamekuwa na tabia ya kuvamia maeneo ambayo yanayopitiwa na miradi
mikubwa na kuyaendeleza kwa kupanda miti na kujenga nyumba ili waweze
kulipwa fidia, Jambo ambalo halitakubalika.
Aliweka wazi kuwa mpaka sasa
tayari wameshapiga Picha za awali katika maeneo yote yatakayopitiwa na
mradi huo ili kurahisisha zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi
watakaoposha mradi huo.
” Kuna baadhi ya wananchi wakiona
mradi mkubwa unapita wanaanza kuweka nguvu kubwa ya kujenga nyumba
ambazo haziishi watu ili mradi tu wategeshe, mwingine anahamisha miti ya
minazi au mkorosho ili afidiwe, hii si sawa !wananchi acheni tabia
hiyo, na kila mmoja awe mlinzi kwa mwenzake na tuelezane ukweli kuhusu
Miradi ya Maendeleo kwa faida yetu sote,” Alisema Lukuvi
Akizungumzia zoezi la ulipaji
fidia, Lukuvi alisema kila mwananchi atayepisha Mradi wa Bomba la
Kusafirisha mafuta ghafi, Serikali haitamuonea mtu yeyote na kila mmoja
atalipwa kile anachostahili kulipwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi
nchini.
Aidha aliwataka Maafisa Ardhi kwa
kushirikiana na Viongozi wa Serikali za Mitaa pamoja na vijiji kutoa
elimu sahihi juu ya ulipaji wa fidia kwa wananchi kwa mujibu wa Sheria
ya ardhi ili kuepusha changamoto zitakazoweka kujitokeza hapo baadaye.
Lukuvi aliweka wazi kuwa katika
zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi viwango vitakavyotumika ni vile
vilivyopo katika sheria ya ardhi ya Tanzania hivyo wananchi waridhike na
kile watakacholipwa kwa wakati huo.
Aidha aliwataka wananchi
kutokwamisha ujenzi wa mradi huo kwa namna moja ama nyingine pia
amewasihi kushirikiana na wale watakaokuwa wakifanya kazi katika maeno
husika ili kurahisisha ukamilishwaji wa ujenzi wa bomba hilo kwa haraka
zaidi kwa kuwa mradi huo una manufaa kwao na taifa kwa ujumla.
“endapo mtu amejenga eneo la
hifadhi ya barabara ambapo bomba hilo litapita hatalipwa fidia, kwa kuwa
fidia itatolewa kwa wale tu ambao maeneo ya yemepitiwa na bomba hilo na
si wale waliovamia maeneo ya hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria
ya ardhi,” alifafanua Lukuvi.
Ujenzi wa Bomba la kusafirisha
mafuta ghafi limeshirikisha Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali
katika kufanikisha ujenzi wake ikiwemo Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Fedha na
Uchumi, Wizara ya Uchukuzi na Mawasiano pamoja na Wizara ya Mambo Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wananchi wote wameaswa kuwa
walinzi wa miundo ya bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima nchini
Uganda hadi eneo la Chongoleani katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment