Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa salamu zake za maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga John Mgeta (wa kwanza kushoto) na Jaji
Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga Dk. Adam
Mambi (wa pili kutoka kulia) na Mwanasheria wa Serikali mkoa wa Rukwa
Prosper Regerera.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.
Joachim Wangabo akisalimiana na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Kanda ya Sumbawanga Dk. Adam Mambi.
………………….
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo amesema maboresho ya TEHAMA yanayofanywa na mhimili wa mahakama
nchini utasaidia kupunguza foleni za wananchi wanaofika ofisi za Wakuu
wa Wilaya na kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta haki zao.
Amesema kuwa kitendo cha mwaanchi
kuweza kujua mwenendo wa kesi bila ya kufika
mahakamani ni maendeleo
makubwa yanayofikiwa na mhimili huo na kuwaasa kuanza kufanya kazi baada
ya kuwa likizo ya mwisho wa mwaka.
Ameyasema hayo kwenye maadhimisho
ya wiki ya sheria ambayo hufanyika tarehe 1, Februari ya kila mwaka
katika Viwanja wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga
inayojumuisha mikoa ya Rukwa na Katavi.
“Mwaka 2018 na jitihada
zilizofanyika na mahakama umekuwa mwanzo mzuri, wananchi watajitokeza
kutafuta elimu hii ya sheria na wanapoipata itatupunguzia msongamano
kwenye ofisi zetu za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ili tufanye kazi za
maendeleo sio kusuluhisha migogo ya ndoa, mirathi na ardhi ambayo yote
imekaa katika misingi ya kisheria,” Alieleza.
Na kuongeza kuwa elimu hii ya
sheria iendelee kutolewa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa
wakati huku wakizingatia kaulimbiu ya maadhimisho hayo inayosema
“Matumizi ya TEHAMA kwa kutoa haki kwa wakati na kuzingatia maadili.”
Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga John Mgeta ametahadahrisha
matumizi mabaya ya Teknolojia katika kuvunja maadili na misingi ya
mahakama na utu kwani watu hutumia teknolojia hiyo kuendeleza rushwa
kupitia namba za simu za mahakama.
“Mtumishi wa mahakama anaweza
kutumia simu kuwasiliana na mtu akimuomba rushwa au kufanya miamala ya
pesa, vyombo vya habari na wananchi ambao wanakiuka maadili kwa kutumia
simu na TEHAMA, sisi tunasisitiza matumizi haya yazingatie maadili,”
Alibainisha.
Awali akitoa taarifa ya chama cha
wanasheria Tanzania Wakili Baltazar Chambi amesema kuwa mahakama ya
Tanzania kwa kutumia TEHAMA itafikia suluhu mojawapo ya uhakika wa
utoaji wa haki kwa wakati kwa kulitambua hilo wadau wa haki ni vyema
wakajua matumizi ya TEHAMA ili kuleta ufanisi katika kazi zao.
No comments:
Post a Comment