Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akizungumza wakati wa
Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana. Wa
pili kushoto ni Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe
akiteta jambo na Naibu Meya Jumanne Ngede. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya
ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo jana.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na
Wageni waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani la
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo
jana.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akizungumza wakati
wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana.
……………..
Na Ramadhani Juma,
Ofisi ya Mkurugenzi
UJENZI wa stendi ya mabasi
kubwa na ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma unatarajiwa kuanza mapema
mwezi Machi mwaka huu katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya Mji wa
Dodoma.
Jumla ekari 50 zimetengwa katika
eneo hilo lililopo mashariki mwa Mji barabra ya Dodoma-Dar es Salaam,
ambapo ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kukamilika baada ya kipindi cha
miei 24.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi wakati wa mkutano wa
Baraza la Madiwani lililofanyika Mjini hapa kwa ajili ya kupokea taarifa
mbalimbali za kimaendeleo zilizotekelezwa katika kipindi cha robo ya
pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 kinachoanzia Mwezi Septemba hadi
Desemba 2018.
Kunambi aliwaambia wajumbe wa
Mkutano huo kuwa, stendi hiyo ni kubwa na ya kisasa yenye hadhi ya Makao
Makuu ya Nchi, na kwamba itakuwa ya mfano kwa Nchi zote za ukanda wa
afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment